Kocha amtema Mnigeria Ogbu Chukwadi
Ogbu Chukwadi |
WAKATI Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts, amemuondoa
kwenye programu zake mshambuliaji wa kimataifa raia wa Nigeria, Ogbu Chukwadi,
timu hiyo inatarajiwa kuweka kambi nje ya nchi.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya klabu hiyo kiliipasha chanzo chetu cha habari kwa sharti la kutotajwa jina kuwa Brandts ameufikishia maoni
uongozi wake kuwa hahitaji kufanya kazi na mshambuliaji huyo ambaye alifanikiwa
kumuona siku moja na kuumia hadi sasa.
Aidha, chanzo hicho kilisema kuwa wakati akiwasilisha
mapendekezo ya kumtema Ogbu, yaliambatana na mahali pa kuweka kambi kwa ajili
ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
“Kocha yeye ndiye hamtaki katika programu zake Ogbu na
tayari ameuambia uongozi, maana anaonekana kutokuwa na umuhimu katika timu yetu
japokuwa anarekodi nzuri kisoka,” alisema mtoa habari huyo.
Aliongeza kuwa kutokana na kumkosa mchezaji huyo, kocha
ameutaka uongozi kuhakikisha wanamtafutia walau washambuliaji wawili, kwa kuwa
kuna upungufu katika safu ya ushambuliaji ambao unahitaji maboresho.
Alisema mapendekezo makubwa ya kocha ni kurudi nchini
Uturuki ambako kuna hali ya hewa nzuri iliyowafanya kutwaa ubingwa msimu
uliopita na kuwa endapo uongozi utashindwa katika nchi hiyo, usake nyingine
yenye hali ya hewa kama hiyo.
Licha ya Brandts kumtema kikosini mwake mchezaji huyo,
siku anawasili, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako, alisema kuwa
huyo si mchezaji bali ni mfanyabiashara mwenzake.