Moyes: Nitasajili wapya Man Utd
KOCHA wa Manchester United, David Moyes amesema atasajili nyota wengine wapya kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili huku akikwepa kuzumgumzia ofa ya pili ya Chelsea kwa Wayne Roooney.
Akizungumza baada ya mechi ya kirafiki kati ya timu yake dhidi ya AIK ya Sweden Jumanne wiki hii iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 mjini Stockholm, alikiri kuwa hajawahi kumuuliza Rooney juu ya ofa ya Chelsea.
“Sijamuuliza. Hupaswi kumlazimisha mtu acheze Manchester United.” Alisema kocha huyo aliyetua Old Trafford Mei mwaka hii akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu baada ya kuinoa miaka 27.
Kauli ya Rooney aliyekosa safari ya Sweden kutokana na majeruhi na ambaye anakosa pia mechi maalumu ya leo ya Rio Ferdinand dhidi ya Sevilla, inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu yake.
“Sidhani kama atacheza mechi ya Ijumaa (leo),” alisema Moyes. “Nayo nafasi, lakini sidhani kama ataweza kucheza. Japo hana maumivu makubwa, tatizo ni kwamba tuna mechi Jumapili, ni jambo la kulizingatia.
“Je, yu fiti kuliko soka yake ya baadaye? Ndio.Tunataka kumwezesha Wayne acheze bila kujali atabaki nasi au ataondoka,” alisema Moyes.
Kwa upande wa sura mpya, awali United ilikuwa ikimhitaji Thiago Alcantara aliyejiunga na Bayern Munich akimfuata kocha wake wa zamani, Pep Guardiola, japo kwa sasa inaendelea kumpigania kumsajili Cesc Fabregas.
Juzi, kuna habari kuwa Moyes alikuwa na mpango wa kumsajili Marouane Fellaini
wa Everton, timu ambayo kocha huyo aliinoa kwa miaka 11 kabla ya kujiunga na Manchester United.
No comments:
Post a Comment