WAGOMBEA 25 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, fomu hizo zilianza kutolewa Agosti 16 na hadi jana, wagombea wawili wamejitosa nafasi ya rais, ambao ni Jamal Malinzi na Omar Nkwarulo huku Makamu wa Rais ni Ramadhani Nasib na Wallace Karia.
Aliwataja waliochukua fomu za kuwania ujumbe kuwa ni Athumani Kambi, Charles Komba, Davis Mosha, Elias Mwanjala, Eliud Mvella ‘Wamahanji’, Epaphra Swai, Farid Nahdi, Hussein Mwamba, Jumbe Magati, Kamwanga Tambwe na Khalid Mohamed.
Wengine ni Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir, Omari Walii, Samwel Nyalla, Shaffih Dauda, Stanley Lugenge, Twahir Njoki, Vedastus Lufano, Venance Mwamoto na Wilfred Kidau.
Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu, aliyechukua fomu ni Hamad Yahya anayewania uenyekiti.
No comments:
Post a Comment