Micho Taifa Stars inaniumiza kichwa
Awakosa Tony Odur na Patrick Edema
WAKATI msfara wa timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars
ukitarajiwa kutua mjini Kampala, Uganda tangu jana mchana, Kocha wa Uganda
Cranes, Sredojevic Milutin Micho, amesema katika mechi hiyo ya Jumamosi vijana
wake watashambulia kwa dakika zote.
Micho ambaye kikosi chake kimeingia kambini juzi kutokana
na yeye kuwa safarini nchini Ethiopia kufuatilia viwango vya nyota wake watatu
wanaochezea St. George ambayo mwishoni mwa wiki ilicheza mechi ya Kombe la
Shirikisho dhidi ya Stade de Malien ya Mali.
Nyota waliompeleka Micho Ethiopia, ni Robert Ssentongo,
Robert Odongkara na Isaac Isinde na kuwashuhudia vijana wake wakiisaidia St.
George kushinda mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya makundi.
"Tutawakabili Stars kwa kuanza kufunga kuanzia
mwanzoni mwa mchezo. Kwa bahati mbaya, hatuna muda.
“Ninachotaka kufanya sasa ni kuwasaidia wachezaji
kujielekeza kwenye mechi. Nitakachofanya ni kuwafundisha kucheza kwenye nafasi
na kufanya kile kisichotarajiwa, kufungua nafasi na kuwadhibiti wapinzani,”
alisema Micho.
Cranes itaikabili Stars ikiwa na tatizo la ufungaji kwani
katika mechi mbili za kirafiki ilizocheza na vijana wa chini ya miaka 23 (U-23
Kobs) na kufungwa zote kwa bao 1-0
ambapo Denis Iguma alicheza sehemu ya kiungo.
Mbali ya ubutu wa safu ya ushambuliaji, pia Micho
atawakosa wachezaji wake wawili wa mbele,
Tony Odur na Patrick Edema. Wakati Odur anauguza nyonga,
Edema amekwenda Ureno kwa majaribio.
Micho amewaita nyota wengine Simon Okwi (KCC FC), David
Kasirye (URA FC) na Henry Oguti anayechezea Kiira Young.
Hata hivyo, Okwi ameitwa licha ya kushindwa kufungia bao
KCC msimu uliopita huku kukiwa na shaka juu ya kiwango cha Kasirye.
No comments:
Post a Comment