Suarez ataka kuteta na Arsenal
JUHUDI za Arsenal kumwania mshambuli wa kimataifa wa
Uruguay anayechezea Liverpool ya England, Luis Suarez huenda sasa zikaanza
kuzaa matunda baada ya nyota huyo kuataka kufanya nao mazungumzo.
Suarez atakayekosa mechi za mwanzoni mwa msimu wa Ligi
Kuu, anaamini dau la pauni mil 40 la Arsenal, linakidhi matakwa ya mkataba
wake.
Suarez anasema kuna uwezekano Liverpool ilitafsiri vibaya
kipengele katika mkataba, hivyo amepanga kumweleza kocha wake
Brendan Rodgers anataka kukutana na Arsenal.
Kauli ya nyota huyo mtukutu, kunahuisha harakati za
Arsenal kumwania mchezaji huyo licha ya ofa zake mbili kutupwa.
Hata hivyo, baada ya Arsenal kushindwa kumpata Gonzalo
Higuain wa Real Madrid ambaye ametimikia Napoli, nguvu zote sasa imeelekeza kwa
Suarez.
Suarez ni miongoni mwa wachezaji wa kutumainiwa katika
kikolsi cha Liverpool, akiifungia mabao 30 katika mechi 44.
Tangu ajiunge na Liverpool Januari, 2011 akitokea
Ajax ya Uholanzi kwa kitita cha pauni
mil 22.7, ameifungia jumla ya mabao m, 51 katika mechi 96.
Kabla ya Liverpool, Suarez aliondoka Ajax baada ya
kuifungia mabao 49 katika mechi 48 huku akiifungia Uruguay mabao 31 katika
mechi 62.
Wakati hayo yakiendelea, uwezekano wa Arsenal kumtwaa
Suarez ni mkubwa baada ya kufikia dau la pauni mil 40 ambalo linaendana na
kipengere cha mkataba.
Liverpool ikikuna kichwa kumbakisha nyota huyo, uwezekano
wa kuondoka ni mkubwa kama Arsena itapanda zaidi ya dau hilo.
Kauli hiyo chungu ya Suarez inakuja siku chache tu tangu
kocha wa Liverpool ashushe pumzi baada ya nyota huyo kujiunga na timu ziarani
Asia na Australia.
Aliungana na wenzake tangu Jumapili iliyopita mjini Melbourne, akitokea kwenye mapumziko baada ya
michuano ya Kombe la Mabara nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment