Garvinho ang’oka Arsenal
KLABU ya AS Roma ya Italia imekaribia kumtwaa nyota wa kimataifa
wa Ivory Coast, Garvinho kwa kitita cha pauni mil 8
akitokea Arsenal ya England.
Hiyo ni kutokana na juhudi za AS Roma waliofunga safari
hadi Emirates kuzungumza na viongozi wa Arsenal kwa siku ya juzi na jana na leo
huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa pande hizo kufikia muafaka.
Kimsingi pande
hizo mbili zimeshafikia muafaka kuhusu dau, kilichokuwa bado kinadiliwa
ni mengine yanayohusu mkataba ikiwemo mshahara kwani Roma wanataka wamlipe pauni 50,000 kwa wiki kama wa Arsenal.
Hesabu za Arsenal ni kumuuza Gervinho kutoa nafasi ya
ujio wa Luis Suarez na Marouane Fellaini japo bado inawaota Cesc Fabregas na
Wayne Rooney.
Ndio maana Gervinho ameachwa katika ziara ya maandalizi
ya msimu ujao barani Asai kwa maelezo
kuwa nyota huyo yu mgonjwa
Presha ya Roma kumtaka Garvinho inachagizwa na
kocha Rudi Garcia, aliyewahi kumnoa nyota huyo kwa msimu
mwili akiwa na Lille ya Ufaransa kabla ya kutua
Arsenal mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment