Liver nayo yawafumua waindonesia 2-0 angalia magoli.
Saturday, July 20, 2013
Mshambuliaji wa Simba, Marcel Boniventure akitafuta mbinu za kumtoka beki wa URA ya Uganda, Walulya Derrick. |
Simba yanyofolewa sharubu U/Taifa
TIMU ya Simba jana ilichapwa mabao 2-1 katika mechi ya
kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA ya Uganda iliyochezwa Uwanja wa Taida,
jijini Dar es Salaam.
Shujaa kwa upande wa URA, alikuwa Lutimba Yayo aliyeifungia
mabao yote katika dakika za 54 na 74, hivyo kuanza vema ziara yao ya mechi za
kirafiki ambapo leo itacheza na Yanga.
Simba walitangulia kupata bao dakika ya saba, likifungwa na Betram Mombeki akitumia uzembe wa mabeki wa URA kukawia kuokoa mpira karibu ya lango.
Simba: Abel Dhaira, Nassor Masoud Chollo, Issa Rashid, Samuel Senkoom, Rashid Juma, Jonas Mkude, Ramadhan Singano,
Wlliam Lucian, Betram Mombeki, Zahor Pazi na Marcel Boniventure.
URA: Bwete Brian, Walulya Derrick, Munaaba Allon, Owino
Joseph, Mugabi Jonathan, Agaba Oscar , Feni Ali, Ngama Emmanuel, Lutinga Yayo,
Kasibanto James na Mugabi Yasin.
Waganda hao leo wanashuka tena dimbani kucheza na mabingwa
wa soka Tanzania Bara, Yanga kwenye Uwanja whuo wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Wewe ndio mchizi wetu |
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, jana
aligeuka shujaa kwenye mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika Bwalo la Maofisa
wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya wanachama
wapatao 700.
Tofauti na dalili za awali pengine mkutano huo ungekewa na
presha kubwa ya wanachama kuhoji mambo mbalimbali ya kiuongozi, mkutano huo
jana uligeuka shangwe na nderemo za wanachama kiasi cha kubariki kila
walichoelezwa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mkutano huo, wanachama
wengi walionesha kuridhishwa na utendaji mzima wa kiongozi wao licha ya kuwepo
changamoto mbali mbali pia wanastahili kuupongeza uongozi uliopo madarakani
chini ya Rage.Baadhi ya wanachama wameomba mabadiliko mbali mbali katika
utendaji wa klabu wakiamini klabu hiyo chini ya Rage, watapata mafanikio
makubwa katika msimu ujao.Jambo jingine ni wanachama kuombwa kuzika tofauti
zilizojitokeza hadi kuibua mgogoro ndani ya klabu hiyo kiasi cha viongozi
kujikuta wakigongana wao kwa wao hivyo timu kushindwa kufanya vizuri.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Rage alisema hatarajii
mapinduzi katika uongozi wake kwani wamekuwa wakichapa kazi kwa mujibu wa
katiba ya klabu hiyo, hivyo msimu ujao
utakuwa ni wa mafanikio kwa klabu hiyo.
“Naaamini mambo yatakwenda vizri katika msimu ujao wa ligi
na timu itafanya vizuri kutokana na mipango na mikakati tuliyojiwekeza,”
alisema Rage na kuongeza wataitisha mkutano mwingine kabla ya Novemba na
kuongeza:
“Tunataka tuwe na sera bora za utawala na utendaji ambapo
kupitia sera hizi kutakuwa na mfumo bora wa utendaji, kiutawala, kimajukumu na
kiuwajibikaji ambapo kila mtu atajikuta anafanya kazi yake,” alisema Rage.
Rage pia amesisitiza msimamo wa kulifuta tawi la Mpira Pesa
kwa hoja wanachama wa tawi hilo wamekuwa
wakienda kinyume na taratibu za klabu hiyo wakitaka kuwa juu ya uongozi na
kusema jambo hilo halikubaliki kamwe.
“Mpira pesa hawako juu ya Klabu ya Simba, bali ndani ya
klabu hiyo, hivyo hatuwezi kuvumilia kuona wanataka kukaa juu ya klabu kitaifa,
suala ambalo ni kinyume na utaratibu kabisa,” alisema Rage.
Rage alibainisha kuwa uongozi uliopo madarakani utaendelea
kuwajibika katika mambo yote licha ya wanachama hao kutaka kujua hatima ya
nafasi ya Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akisema nafasi hiyo
imezibwa na Joseph Itang’are ‘Kinesi.’
Katika mkutano huo ulidumu kwa dakika 60, agenda zilikuwa
kuthibitisha kumbukumbu ya mkutano uliopita, hotuba ya Mwenyekiti na kupokea na
kujadili taarifa za kazi kutoka kamati ya utendaji.
Nyingine ni kudhibitisha hesabu za fedha zilizokagaliwa za
mwaka uliotangulia, kuthibitisha taarifa za chombo cha ukaguzi na hatua
zilizochukuliwa na vyombo
vya utendaji na kudhibitisha bajeti kwa mwaka ujao.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huo majira ya saa 5 asubuhi,
ndipo ukumbi ukagubikwa na shangwe za wanachama wakiupngeza uongozi wa klabu
hiyo
hadi kumbeba Ragea akionekana ni shujaa.
Hitimisho hilo lilikwenda sambamba na wanachama
waliohudhuria mkutano huo, kupewa tiketi ya kuingilia uwanja wa Taifa kujionea
mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Simba na URA ya Uganda.
Kuelekea mkutano huo, baadhi ya wanachama walikuwa wakihoji
uhalali wa mkutano huo wakidai umeitishwa kinyume cha katiba na wakapanga
kwenda mkutanoni kuung’oa.
Mourinho na Terry |
Mourinho amtisha
Terry
NAHODHA wa Chelsea,
John Terry ana kibarua kigumu cha kupigania majaaliwa yake klabuni Stamford
Bridge.
Kocha mpya wa
mabingwa hao wa Europa League, Jose Mourinho amemwambia nyota huyo muhimu na
kiongozi wa kweli dimbani kuwa anapaswa kuthibitisha ubora wake kikosini.
Mourinho alisema:
“Terry hayuko salama na mwenyewe analitambua hilo. Jambo pekee ambalo anajua
liko salama ni urafiki wetu na mahusiano yetu.
“Tumezungumza kuhusu
hilo na kimsingi anatambua kwa ukamilifu kabisa kwamba urafiki ni urafiki na
biashara baina yetu ni jambo jingine kabisa. Hii ni biashara hivyo, ndiyo, yeye
anatakiwa kuboresha kiwango na uwajibikaji wake.
“Mimi kamwe siwezi
kumlinda wala kumpa upendeleo kikosini mbele ya mwingine yeyote – na
analitambua hilo kwa sababu anajua asili yangu,” alisisitiza Mourinho aliyeihama
Real Madrid na kurejea Chelsea.
Terry, 32, ni beki
wa kati aliyebakisha miezi 12 katika mkataba wake wa sasa na klabu hiyo na
Mourinho anamtaka kukabiliana vema na changamoto kuhakikisha anathibitisha
ubora wake ili aweze kuambulia mkataba mpya.
Mreno huyo
aliongeza: “Kutokana na muonekano wa kimwili katika ubora, Terry anahitaji
kufanya kazi kwa bidii na hapaswi kupata majeruhi kwa sababu majeraha yanavunja
mageuzi ya mchezaji yeyote.
“Kwangu mimi, hiyo
ndiyo hatua ya msingi kwa Terry. Anapaswa kuimarisha na kuthibitisha ubora wake
kama mwingine yeyote,” alisema Mourinho kwa msisitizo.
Mo Farah |
Mo Farah avunja
rekodi
BINGWA medali mbili
za dhahabu za mashindano ya Olimpiki ya majira ya joto 2012, Mo Farah ameibuka
mshindi wa pili wa mbio za Diamond League jijini hapa, huku akivunja rekodi ya
mita 1,500 iliyodumu kwa miaka 28 ya mkimbiaji Steve Cram.
Farah, Mwingereza
mwenye asili ya Somalia, amejiwekea rekodi ya kuwa mtu wa sita kwa kasi duniani
katika umbali huo, baada ya kutumia muda wa dakika tatu na sekunde 28.81,
unaomfanya kushikilia rekodi miongoni mwa wakimbiaji barani Ulaya.
Farah, bingwa wa
medali za dhahabu katika mbio za mita 5,000 na 10,000 za Olimpiki ya jijini
London mwaka jana, alikuwa wa pili nyuma ya Mkenya Asbel Kiprop, ambaye alikimbia
muda rekodi inayoongoza duniani wa dakika 3:27.72.
“Nimeridhishwa na
matokeo na kimsingi kulikuwa na ushindani mkubwa katika mchuano huu,” alisema
Farah, 30, baba wa watoto wawili pacha.
Cram, aliyekuwa
akishikilia rekodi ya dunia, ambaye alitumia muda wa dakika 3:29.67 ambao ni
rekodi kwa wakimbiaji raia wa Uingereza iliyodumu tangu Julai 16, 1985, alikiri
kushangazwa na kasi ya Farah katika mbio hizo.
Muda huo pia
unaingia katika rekodi binafsi za wakimbiaji wa kudumu Sebastian Coe aliyetumia
dakika 3:29.77 mwaka 1986 na Steve Ovett (3:30.77) mwaka 1983 ambao walikamata
nafasi za pili na tatu miongoni mwa Waingereza kwenye mbio za mita 1,500.
Farah alikuwa katika
mbio alizozichukulia kama kipimo binafsi kuelekea mbio za ubingwa wa dunia
mwezi ujao jijini Moscow, ambako atakimbia kwenye mbio za mita 5,000 na 10,000.
Hakuwa na matarajio yoyote kuweka rekodi ya kutazamwa.
Luis Suarez |
Madrid yaiharibia Arsenal kwa Suarez
WAKATI mshambuliaji
Luis Suarez akiwakabili Liverpool kufanya nao mazungumzo ya ana kwa ana kuomba
ridhaa ya kuhama, imeelezwa kuwa Arsenal wanakabiliwa na vita ya pili na Real
Madrid, baada ya miamba hiyo kujitosa kuwania saini ya nyota huyo.
Madrid wanajiandaa
kutuma ofa ya pauni milioni 20 pamoja na mshambuliaji wake wa kimataifa wa
Argentina, Gonzalo Higuain, ili kupata saini ya Suarez nyota wa kimataifa wa
Uruguay.
Mfaransa anayeinoa
Arsenal, Arsene Wenger, amekuwa na mawindo mawili kwa pamoja ya kuwanasa Suarez
na Higuain, lakini uamuzi huo wa Madrid unaiweka Gunners katika hatari ya
kuwakosa wote kwa pamoja.
Washika Bunduki hao
wa London walikuwa na imani kubwa ya kufanikiwa kupata saini ya Suarez kutoka
Liverpool, baada ya kuboresha ofa yao kwa nyota huyo na kufikia kitita cha
pauni milioni 40.
Gunners ilikuwa
ilipandisha dau hilo kutoka ofa ya awali ya pauni milioni 35 zilizokataliwa na kocha Brendan Rodgers,
aliyesisitiza kuwa hayuko tayari kumuuza mtikisa mabao wake huyo mwenye umri wa
miaka 30 chini ya dau la pauni mil. 55.
Tayari Gunners
ilishakubali kumlipa Suarez mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki kumng’oa mkali
huyo Anfield.
Suarez, hata hivyo,
anadaiwa kupendelea kutua Madrid kuliko Arsenal, akiwa na nia ya kukimbia
jinamizi la matukio tata dimbani katika soka la England.
Na sasa Madrid
inamthaminisha Higuain kwa dau la pauni milioni 35 baada ya kupokea ofa ya
thamani hiyo kutoka Napoli, ambapo inajiona iko sahihi kuongeza dau la pauni milioni
20 kukamilisha kitita cha pauni milioni 55 zinazotakiwa na Rodgers.
Gerardo Martino ‘Tata’ |
Gerardo kumrithi
Vilanova
KOCHA wa zamani wa timu
ya taifa ya Paraguay, Gerardo Martino
‘Tata’ anapewa nafasi kubwa ya kuziba nafasi ya Tito Vilanova, aliyejiweka
kando kutokana na sababu za kiafya.
Vilanova (44),
aliyekuwa ametwa nafasi hiyo baada ya kuondoka kwa Pep Guardiola, amekuwa
akisumbuliwa na kansa ya koo kwa muda mrefu.
Kuna habari kuwa,
Martino mwenye umri wa miaka 50, alitarajiwa kwenda nchini Hispania kwa
mazungumzo ya kazi hiyo.
Martino, aliyeipa
Newell's Old Boys ubingwa wa Argentina msimu uliopita, kwa sasa yupo nje ya
mkataba na wakali hao.
Ni kocha mwenye
rekodi ya kubeba ubingwa wa Paraguay na mwaka 2007, alitwaa tuzo ya Kocha Bora
Amerika Kusini.
Kocha huyo
aliyezaliwa Novemba 20, 1992, pia amewahi kufundisha Brown de Arrecifes,
Platense, Instituto, Libertad, Cerro Porteño, Colón, Libertad na timu ya taifa
ya Paraguay kuanzia 2006 hadi 2011.
PAMOJA na Makamu Raia wa Barcelona , Josep
Maria Bartomeu, kusema kamwe kiungo wao Cesc Fabregas hauzwi, Klabu ya Manchester United
imeongeza kasi ya kumngoa Santiago Bernabeu.
Kocha wa United, David Moyes,
aliyasema hayo jana baada ya timu yake kushinda 5-1 katika mechi ya kirafiki
dhidi ya A-League All Stars.
Alitumia nafasi hiyo
kusisitiza kuwa, United imewasilisha ofa ya pauni mil 30, hivyo wanasubiri jibu
kutoka Barcelona .
Wakati United ikiwa na
mipango hiyo, nyota wake mahiri Robin van Persie, alisema jana anamkaribisha Fabregas kwa mikono mwili.
“Ni mchezaji mzuri,” alisema
Fabregas alipozungumza na Channel Seven, licha ya kukiri hajawahi kuzungumza
naye.
Subscribe to:
Posts (Atom)