Wednesday, July 24, 2013

Kocha amtema Mnigeria Ogbu Chukwadi
Ogbu Chukwadi
WAKATI Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts, amemuondoa kwenye programu zake mshambuliaji wa kimataifa raia wa Nigeria, Ogbu Chukwadi, timu hiyo inatarajiwa kuweka kambi nje ya nchi.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya klabu hiyo kiliipasha chanzo chetu cha habari kwa sharti la kutotajwa jina kuwa Brandts ameufikishia maoni uongozi wake kuwa hahitaji kufanya kazi na mshambuliaji huyo ambaye alifanikiwa kumuona siku moja na kuumia hadi sasa.
Aidha, chanzo hicho kilisema kuwa wakati akiwasilisha mapendekezo ya kumtema Ogbu, yaliambatana na mahali pa kuweka kambi kwa ajili ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
“Kocha yeye ndiye hamtaki katika programu zake Ogbu na tayari ameuambia uongozi, maana anaonekana kutokuwa na umuhimu katika timu yetu japokuwa anarekodi nzuri kisoka,” alisema mtoa habari huyo.
Aliongeza kuwa kutokana na kumkosa mchezaji huyo, kocha ameutaka uongozi kuhakikisha wanamtafutia walau washambuliaji wawili, kwa kuwa kuna upungufu katika safu ya ushambuliaji ambao unahitaji maboresho.
Alisema mapendekezo makubwa ya kocha ni kurudi nchini Uturuki ambako kuna hali ya hewa nzuri iliyowafanya kutwaa ubingwa msimu uliopita na kuwa endapo uongozi utashindwa katika nchi hiyo, usake nyingine yenye hali ya hewa kama hiyo.
Licha ya Brandts kumtema kikosini mwake mchezaji huyo, siku anawasili, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako, alisema kuwa huyo si mchezaji bali ni mfanyabiashara mwenzake.

No comments:

Post a Comment