MCHEZAJI Gareth Bale wa Tottenham amemalizana na Klabu ya Real Madrid juu ya dau ili atue Santiago Bernabeu baada ya kujiunga nayo na kilichobaki ni klabu husika kufikia muafaka kuhusu ada ya uhamisho.
Kuna habari kuwa, klabu hizo mbili bado zipo kwenye mazungumzo ya mwisho kuhusu nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, japo Real Madrid ilishatoa ofa ya pauni mil 86.
"Hata kama mazungumzo baina ya klabu hizo mbili yatachukua siku kadhaa, hiyo itakuwa ni kutimiza wajibu tu kwani Real Madrid na Bale wameshafikia muafaka juu ya maslahi," alisema Mwandishi Mwandamizi wa BBC, Dan Roan na kuongeza:
"Makubalinom binafsi kati ya Real Madrid na Bale, yameshafikiwa, hivyo hakuna kikwazo tena cha uhamisho, unaweza kutangazwa wakati wowote."
Ofa iliyowasilishwa na Real Madrid kwa Tottenham kinapiku ya pauni mil 80 iliyomng’oa Cristiano Ronaldo mwaka 2009 kutoka Manchester United hadi Santiago Bernabeu Bale mwenye rekodi ya kucheza mechi 146 za Ligi Kuu ya England na kufunga mabao 42, amelimwa kadi 15 za njano na moja nyekundu na kuichezea timu ya taifa ya Wales mara 41.
"Mazungumzo kati ya mchezaji na klabu ni tofauti nay ale ya Klabu na Klabu kuhusu dau la uhamisho," aliongeza Roan na kusisitiza:
"Kilichobaki ni taratibu za kawaida tu kwa Spurs kukubali ofa ya Real Madrid kisha kutangaza rasmi kuwa jambo hilo limefika mwisho.
Bale aliyetua Spurs mwaka 2007 kwa kitita cha pauni mil 10 akitokea Southampton, mwaka huo akawa nyota bora na Chama cha Wanasoka wa Kulipwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo, akifunga mabao 26.