Demba Ba namuogopa Rooney Chelsea
MSHAMBULIAJI, Demba Ba, amekana taarifa kuwa
anajiandaa kutimka klabuni Stamford Bridge , kukimbia ujio wa Wayne Rooney kama Chelsea itafanikiwa kupata saini ya nyota huyo wa
kimataifa wa England .
Badala yake, Ba nyota wa kimataifa wa Senegal
amemkaribisha kwa mikono miwili, Rooney anayechezea Manchester United, huku
akiongeza kuwa Darajani ni sehemu sahihi ya ushindani na yu tayari kwa vita ya
namba.
Ba ameongeza kuwa anawakaribisha wakali zaidi wa
safu ya mbele klabuni hapo, ili kuwaongezea nguvu yeye, Fernando Torres na
Romelu Lukaku.
“Nadhani tunahitaji ushindani na tunawakaribisha
washambuliaji na wachezaji bora katika kikosi chetu. Ushindani kikosini
utanifanya mimi kuwa bora dimbani kwa kila namna.
“Bila shaka wachezaji wote wanataka kucheza, si
tu washambuliaji wa kati. Lakini tutafanya kazi kwa pamoja kama
timu katika huo huo, kwa manufaa na ustawi wa klabu, kujaribu na kushinda
michezo. Hivyo basi, ndiyo nitabaki hapa hata akija Rooney.”
Ba alifunga moja ya mabao ya Chelsea katika ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya
Indonesia XI juzi usiku mbele ya mashabiki wapatao 65,000 na amekiri kuwa
itakuwa na msisimko wa aina yake kwake kucheza msimu huu chini ya kocha mpya
Jose Mourinho.
Aliongeza kuwa: “Daima inakuwa ni jambo zuri mno
kufunga, lakini katika hatua hii zaidi inakuwa ni kuhusu kuwajibika na kukaza
msuli ipasavyo dimbani ili kurejea hali uhatari kama
ilivyokuwa huko nyuma.
“Najisikia vizuri. Imekuwa
wiki nzuri kikazi chini ya kocha mpya. Tutaona mambo yatakuwaje katika wiki
chache zijazo. Itakuwa hali ya kusisimua sana ,”
alitamba Ba
No comments:
Post a Comment