Arsenal yaendelea kutoa dozi Asia
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia goli |
Timu ya Arsenal inaendelea na wimbi la ushindi mnono katika ziara ya kujiandaa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu England, kwa mara nyingine tena imeipiga Nagoya Grampus Eight ya Japan kwa jumla ya mabao 3-1.
Mabao hayo yakitiwa kambani na Olivier Giroud, Walcott na mjapani wao anaikipiga Arsenal Ryo Miyaichi.
Kwa ushindi huo wapiga bunduki hao wa London wamefikisha jumla ya ponti 9 na mabao 17. Je, kwa kasi hiyo wataendelea nayo mpaka kwenye ligi au ndiyo nguvu ya soda?