Wednesday, July 24, 2013

Higuain apasi vipimo Napoli
Gonzalo Higuain chini ya ulinzi mkali
MSHAMBULIAJI wa Gonzalo Higuain wa Real Madrid ametanguliza mguu mmoja Napoli ya Italia baada ya kupasi vipimo vya afya na kwa hivyo Napoli imesema itamtambulisha rasmi siku ya J,tatu usiku.
 Napoli imekubali kulipa kitita cha euro mil 42.3 kama gharama ya uamisho wake kutoka Madrid
Mbali ya dau hilo, nyota huyo raia wa Argentina atakayekuwa chini ya Kocha Rafael Benitez, atakuwa akilipwa mshahara wa euro 163,000 kwa wiki chini
Awali, Napoli walishatoa ofa ya euro milioni 37, lakini sasa imefikia kiwango hicho kutokana na gharama nyinginezo za mchezaji binafsi.
Baada ya majadiliano ya kina baina ya pande zote, jambo hilo limefika mwisho ambapo nyota huyo atang’oka Santiago Bernabeu kwa kitita hicho cha euro mil 42.3
Higuain anangoka licha ya kocha mpya wa Real Madrid, Carlo Ancelotti hivi karibuni kusema kuwa mchezaji huyo asingeondoka, lakini jana alimwacha nyota huyo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Lyon.
Jeuri ya Napoli katika usajili, inatokana na mauzo
ya Edinson Cavani aliyetua Paris Saint-Germain kwa kitita cha euro mil 63.
Kwa nyota huyo kwenda Napoli, kumefuta juhudi za Arsenal kumwania nyota huyo ambayo baada ya kuona ugumu, iliahirisha jambo hilo hadi Juni.

No comments:

Post a Comment