Tuesday, September 24, 2013

Carlo Ancelotti ajifariji kwa Mesut Ozil

Carlo Ancelotti ajifariji kwa Mesut Ozil
MABAO 15 yaliyofungwa na Real Madid katika mechi nne za mwisho, yamempa kiburi kocha Carlo Ancelotti akisema hawezi kumkumbuka Mesut Ozil aliyetimkia Arsenal ya England.
Ancelotti anasema hana sababu ya kufanya hivyo kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Coentrao na Varane katika kikosi hicho, mabingwa mara tisa wa Ulaya.
Anaamini kuondoka kwa Mesut Ozil kwenda Arsenal, bado hakujaathiri uwezo wa kikosi chake dimbani, akijivunia ushindi wa kishindo wa 6-1 dhidi ya Galatasaray 6-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na 4-1 dhidi ya Getafe.

Perez: Euro mil 100 kwa Bale, si chochote

Perez: Euro mil 100 kwa Bale, si chochote

PAMOJA na ukweli kuwa Gareth Bale kwa sasa ndie mwanasoka ghali duniani baada ya kujiunga na Real Madrid kwa kitita cha euro mil 100 akitokea Tottenham ya England, Rais Florentino Perez amesema ni fedha kiduchu.
Perez, kiongozi anayefahamika kwa sera yake ya kununua nyota wa bei kubwa, amesema japo kiasi hicho kinaonekana kikubwa, lakini fedha hiyo hailingani na thamani yake halisi kwa maana ya uwezo wake dimbani.
Alisema kiasi cha fedha walizotoa kumpata nyota huyo kwenda Santiago, ni kutokana na ukweli kuwa wasingeweza kwenda mbali zaidi ya hapo japo uwezo na thamani halisi ya mchezaji huyo ni zaidi ya kiasi hicho.
"Ukiangalia uwezo wake halisi dimbani na fedha tuliyomnunulia, naweza kusema Bale ametua Madrid kwa bei chee," alisema kiongozi huyo alipozungumza na Cadena SER na kuongeza:
"Kusajili mchezaji kwa kiwango kikubwa ni filosofia ya klabu hii kwa sababu tunaamini ndiye bora kwa msimu huu. Tumekuwa tukimfuatilia kwa miaka miwili.
"Awali, Tottenham hawakutana kumuuza, lakini tuliposikia Manchester United wanamtaka, tukaketi nao kujadili. Hata hivyo kiu yake ya siku moja kucheza Real Madrid tangu akiwa mtoto, ikawa siraha kwetu," alisema.
Tangu Bale atue Real Madrid, amecheza mechi moja dhidi ya Villarreal na kufunga bao, lakini akikosa mechi ya wikiendi iliyopira dhidi ya Getafe kutokana na maumivu ya paja.
Maumivu hayo ya paja yamemzuia Bale kucheza mechi ya leo ya La Liga dhidi ya Elche, lakini huenda akwa fiti kuelekea mechi itakayofuata dhidi ya watani wao wa jadi, Atletico Madrid.

Van Persie kuwakosa Liverpool kesho

Van Persie kuwakosa Liverpool kesho
KOCHA wa Man United, David Moyes amesema hatomjumuisha kikosini mshambuliaji wake Robin Van Persie kwenye mechi ya Kombe la Ligi kati yao na Liverpool.
Van Persie atalazimika kuikosa mechi ya pili mfululizo baada ya kuumia katika mazoezi muda mchache kabla ya mpambano na wapinzani wao wa jadi Manchester City mchezo uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuangukia pua kwa mabao manne kwa moja kutoka watani wao.
"Sifikiri kama Robin Van Persie atacheza siku ya Jumatano na Liverpool, ila anaweza kucheza siku ya Jumamosi katika mechi ya ligi na Timu ya West Brom." amesema Moyes