Friday, August 23, 2013

Raul arudi Santiago Bernabeu,
afunga bao na jezi ya Cristiano

NYOTA wa zamani wa Real Madrid, Raul Gonzalez, jana usiku alirejea Santiago Bernabeu akivalia jezi yake No 7, aliyokuwa akivalia kabla ya kutimkia Al Saad ya Qatar, ambayo sasa inavaliwa na Cristiano Ronaldo.
Raul alipata fursa ya kuvalia jezi hiyo katika mechi ya kirafiki baina ya timu hizo mbili ambapo alichezea timu zote mbili, dakika 45 kila moja na kuifungia Real Madrid bao dhidi ya timu yake ya sasa, Al Saad.
Katika mechi hiyo ya aina yake ya kuwania kombe la Santiago Bernabeu, Raul mwenye umri wa miaka 36, alionesha kiwango bora huku akibubujikwa na machozi, baada ya filimbi ya mwisho.
Akiwa kwenye jezi namba 7, Raul aliwapungia na kuukisi umati baada ya kuifungia bao Real Madrid kutokana na pasi nzuri ya Angel Di Maria.
Kabla ya kuanza kwa mechi hiyo, Raul alipata mapokezi ya aina yake kutokana na kuifanyia makubwa timu hiyo kabla hajaondoka huku akipewa mshipi wa unahodha na kipa, Iker Casillas.
Wakati wa mapumziko, Raul akiwa na jezi na 7, alikimbia hadi kwa mmiliki wa jezi hiyo kwa sasa, Cristiano Ronaldo, ambaye katika kipindi cha kwanza katika mechi hiyo, alivalia jezi namba 11.
Walipokutana, wawili hao walikumbatiana kwa furaha na kuzungumza machache kabla ya Raul kwenda kuvalia jezi ya Al-Saad kwa kipindi cha pili.
Hata hivyo, mechi hiyo iliisha vijana wa Carlo Ancelotti kuiwezesha Real Madrid kutwaa Kombe la Santiago Bernabeu mara ya tisa mfululizo kwa ushindi wa mabao 5-0.
Mabao ya wenyeji yalifungwa na Isco goal, Benzema aliyefunga kwa penalti huku Jese akifunga mawili.
Raul alitimkia Qatar mwaka 2012, baada ya kucheza misimu miwili katika klabu ya Schalke ya Ujerumani.
Mashabiki wa Real Madrid wamekuwa wakimheshimu Raul kutokana na  mchango wake mkubwa, akiongoza kwa ufungaji wa mabao, akicheka na
nyavu mara 323 katika mechi 741.

Miamba 14 kuanza Ligi Kuu Bara kesho

Miamba 14 kuanza Ligi Kuu Bara  kesho

KIVUMBI cha Ligi Kuu Tanzania bara kinaanza kutimka kesho kwa miamba 14 kuanza kampeni ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo msimu wa 2013/14 huku bingwa mtetezi, Yanga akianza na Ashanti United ya Ilala kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga chini ya kocha wake Ernie Brandts iinayoshuka dimbani ikitoka kutwaa Ngao ya Jamii

kwa kuifunga Azam FC bao 1-0 Agosti 17, itakuwa ikipigania ushindi ili kuanza vema ligi hiyo  inayodhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom-Tanzania.
Wakati Yanga ikiwa na hesabu hizo, Ashanti United ‘Wazee wa miba,’ watakuwa wakipambana vilivyo kushinda kudhihirisha uwezo wao kisoka uliowafanya warejee Ligi Kuu pamoja na Rhino Rangers ya Tabora na Mbeya City ya Mbeya.
Yanga, bingwa mara 24 tangu mwaka 1965 ikianzia kampeni Uwanja wa Taifa, mtani wake Simba anayesaka ubingwa wa 18, atakuwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora kuwakabili wanajeshi wa Rhino Rangers wanaocheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwao mwaka 1994.
Simba chini ya Kocha Mkuu Abdallah King Kibadeni, atakuwa na kazi ya kusaka ushindi wa ugenini katika mechi hiyo inayotarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi waliokosa ligi hiyo kwa miaka 12, tangu kushuka daraja kwa timu ya Milambo FC iliyowahi kuwika na kutikisa katika enzi zake.
Wakati Simba ikisaka ushindi ili kuanza vema kampeni ya kutaka kutwaa ubingwa kusawazisha makosa ya kuangukia nafasi ya tatu msimu uliopia, Rhino Rangers chini ya Kocha wake Sebastiani Nkoma, watakuwa wakipambana kudhihirisha uwezo mbele ya mashabi na wakazi wa Tabora.
Akizungumza kuelekea mechi ya leo, Meneja ya Rhino Rangers, Marijan Idd Lukongo alisema hawakupanda daraja ili kuwa wasindikizaji bali kuleta ushindani wa kweli katika Ligi Kuu kwa
lengo la kutwaa ubingwa kama Tukuyu Stars mwaka 1986.
“Tumekuja kuwashika, hatukupanda Ligi Kuu kwa kubahatisha…kwa uwezo, tutapambana
kunatoa upinzani wa hali ya juu. Tunaomba sapoti ya mashabiki kwani tuna uhakika sio kubaki
tu, bali kufanya vizuri kama si kutwaa ubingwa kama Tukuyu Stars 1986,” alisema
Nje ya watani wa jadi, mabingwa mara mbili wa ligi hiyo, Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro itakuwa
nyumbani Manungu kuwakaribisha Azam FC, mechi inayotarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa kutokana
na uwezo wa timu zote mbili.
Azam inayotokea kufungwa bao 1-0 na Yanga katiuka mechi ya Ngao ya Janii, itakuwa na kazi ya kuonesha na kudhihirisha matunda ya kambi ya wiki mbili nchini Afrika Kusini ambako ilicheza mechi nne za kirafiki dhidi
ya Mamelodi Sandowns, Kaizer Chiefs, Moroka Swallows na
Mechi nyingine leo ni katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha kwa maafande wa JKT Oljoro kuwakaribisha Coastal Union ya Tanga huku Magambo JKT ya Tanga, ikiwa mwenyeji wa JKT Ruvu
kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Wageni katika msimu huu, Mbeya City chini ya kocha wake Juma Mwambusi, leo itakuwa kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Edward Moringe Sokoine, kuwakaribisha Kagera Sugar waliomaliza msimu uliopita wakiwa nafasi ya nne chini ya Kibadeni,
safari hii wakiwa chini ya Jackson Mayanja, raia wa Uganda.
Vita nyingine itakuwa kwenye Uwanja wa Mabatini, Kibaha, Pwani kwa maafande wa Ruvu Shoooting kuwakaribisha maafande wenzao wa Tanzania Prisons katika mechi inayotarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa timu hizo.
Raundi ya pili wa ligi hiyo utachezwa Agosti 28, kabla ya kupitisha mechi za mchujo fainali za Kombe la Dunia kati ya Gambia na Tanzania, Taifa Stars  itakayochezwa Septemba 7, mjini Banjul huku raundi ya tatu ikiendelea Septemba 14.

Azam, Simba yaibeba Tanzania FIFA

Azam, Simba zaibeba Tanzania FIFA
Kama ulikuwa hujui kuwa hizi Klabu mbili, Azam na Simba, ndizo zinazotambulika 
katika viwango vya soka ngazi ya klabu duniani ukweli ndio huo.
hii hapa chini ni chati inayowaonesha nafasi zilipo klabu hizo.

Diego Godin afurahia Messi kuumia

Diego Godin afurahia Messi kuumia
Diego Godin
Diego Godin mwenye jezi namba 2 akifurahia kimyakimya
USEMI wa adui yako muombee njaa, ulidhihirika juzi pale Lionel Messi wa Barcelona alipoumizwa hadi kutoka ndani ya kipindi cha kwanza walipocheza na Atletico Madrid katika mechi ya Super Cup iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.

Katika mechi hiyo ya kwanza Super Cup iliyochezwa uwanja wa Vicente Calderon, kabla ya Messi kutoka, Diego Godin alionekana kupeana maelekezo kwa mchezaji mwenzake Miranda wapi amgonge asiendelee na mchezo huo.
Katika kutimiza kilichopangwa, Messi alichezewa rafu na Miranda kiasi cha kushindwa kurejea kipindi cha pili huku nafasi yake ilizibwa na Cesc Fabregas kutokana na kupata maumivu ya mgongo na paja la kushoto.
Yaonesha wazi Godin ambaye ni beki wa Atletico Madrid, alifurahia kutorejea kipindi cha pili kwa kugonga mikono na Miranda kama ishara ya kumpongeza kwa kazi nzurialiyofanya.
Kwa upande wa Messi, si mara ya kwanza kwake kupata maumivu kama hayo kwani katika msimu uliopita, alikabiliwa na maumivu ya bega la kulia.
Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Andoni Zubizarreta, alisema maumivu ya Messi yametokana na kukanyagwa, hivyo kuongeza maumivu mguu wa kushoto aliopata maumivu madogo katika mechi ya ufunguzi wa La Liga, walipoifunga Levante 7-0.
Katika mechi hiyo, Neymar aliyetokea benchi ndie aliisawazishia Barcelona kutokana na krosi ya Dani Alves akisawazisha bao la David Villa, aliyewahi kuchezea Barcelona.
Bao la kichwa la Neymar, lilifungwa kishujaa kiasi cha kumshangaza Andoni, akisema alipiga kichwa kwenye mazingira yasiyotarajiwa.