Tuesday, August 27, 2013

Mourinho ampa Wayne Rooney saa 48 kuamua

Mourinho ampa Rooney saa 48 kuamua
 
 
 
MRENO Jose Mourinho amempa Wayne Rooney muda wa saa 48 awe ametoa jibu ramsi kama atahama Old Trafford na kwenda Stamford Bridge ama vipi.
Mourinho ameamua hivyo, licha ya kocha wa Man Utd, David Moyes kuwahi kutamka bayana kuwa hayuko tayari kumtoa nyota huyo kwa bei yoyote.
Aidha, Mourinho amesisitiza hilo siku moja tu tangu timu hizo zivune sare ya bila kufungana katika mechi ya Ligi Kuu, ikiwa ya pili kwa kila timu tangu kuanza kwa ligi hiyo Agosti 17.
Hayo yote kutokana na Rooney kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mechi hiyo.
Aidha, Mourinho amemwaga sumu hiyo wakati ambao Rooney (27), akionesha wazi kuwa
anataka kuondoka kutokana na mazingira halisi ya Old Trafford kwa sasa juu ya nafasi yake kwenye kikosi chini ya Moyes.
"Kwa namna moja au nyingine, aseme kama anataka kubaki au kuondoka," alisema Mourinho aliyerejea Stamford Bridge msimu huu akitokea Santiago Bernabeu.
Tangu Rooney atue Old Trafford mwaka 2002 akitokea Everton, ameifungia Manchester United jumla ya mabao 156, hivyo kuwa miongoni mwa nyota muhimu katika safu ya ushambuliaji.
Alipoulizwa kuhusu nyota wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto’o wa klabu ya Anzhi Makhachkala, alisema hilo pia litajulikana baada ya masaa 48.
"Kwa kocha kama mimi, klabu kama Chelsea na watu wafanyai kazi pamoja nami, hatutaki kupoteza muda kwa mchezaji wa klabu asiyotaka kumuuza,” alisema Mourinho aliyewahi kuipa Chelsea ubingwa wa Ligi Kuu.

Euro mil 100 zamng'oa Bale

Euro mil 100 zamng'oa Bale

KLABU ya Real Madrid na Tottenham zimeafikiana juu ya nyota wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale aende Santiago Bernaneu kwa kitita cha euro mil 100.
Kiasi hicho kinazidi kile kilichotolewa na klabu hiyo mwaka 2009 kwa Cristiano Ronaldo kumng’oa Old Trafford kwa euro mil 93.
Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy, alisema juzi mpango huo umefanikiwa baada ya majadiliano ya kina baina ya klabu hizo mbili.
Japo Real Madrid ilikuwa bado haijapata uhakika wa nyota huyo, Alhamisi iliyopita mashabiki wa Santiago Bernabeu walikuwa na fulana zenye jina la Bale na11.
Kuna habari kuwa, tayari klabu hiyo imeanza kujenga jukwaa rasmi ambalo litatumika kwa utambulisho wa mchezaji huyo kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Habari zinasema licha ya klabu hiyo kufanya maandalizi ya utambulisho wa Bale, yaelezwa presha yake haiwezi kulinganishwa na yale ya Cristiano Ronaldo, Kaka au  Karim Benzema.