Nani aongeza miaka mitano Man United
KLABU ya Manchester United, imemwongezea nyota wake Nani miaka mitano ya kubaki Old Trafford, alikojisajili tangu mwaka 2007 kwa kitita cha pauni mil 17, akitokea Sporting Lisbon ya Ureno.
Kwa mkataba huo, nyota huyo raia wa Ureno aliyecheza mechi tatu za Ligi Kuu kwa mwaka huu, ataendelea kuichezea Old Trafford hadi mwaka 2018.
Nani ameongezewa mkataba wake akibakisha mwaka mmoja kabla ya mkataba wake wa awali kufika kikomo huku akiwindwa na Juventus, Monaco, Galatasaray, Zenit St Petersburg na Anzhi Makhachkala.