Luis Suarez |
Madrid yaiharibia Arsenal kwa Suarez
WAKATI mshambuliaji
Luis Suarez akiwakabili Liverpool kufanya nao mazungumzo ya ana kwa ana kuomba
ridhaa ya kuhama, imeelezwa kuwa Arsenal wanakabiliwa na vita ya pili na Real
Madrid, baada ya miamba hiyo kujitosa kuwania saini ya nyota huyo.
Madrid wanajiandaa
kutuma ofa ya pauni milioni 20 pamoja na mshambuliaji wake wa kimataifa wa
Argentina, Gonzalo Higuain, ili kupata saini ya Suarez nyota wa kimataifa wa
Uruguay.
Mfaransa anayeinoa
Arsenal, Arsene Wenger, amekuwa na mawindo mawili kwa pamoja ya kuwanasa Suarez
na Higuain, lakini uamuzi huo wa Madrid unaiweka Gunners katika hatari ya
kuwakosa wote kwa pamoja.
Washika Bunduki hao
wa London walikuwa na imani kubwa ya kufanikiwa kupata saini ya Suarez kutoka
Liverpool, baada ya kuboresha ofa yao kwa nyota huyo na kufikia kitita cha
pauni milioni 40.
Gunners ilikuwa
ilipandisha dau hilo kutoka ofa ya awali ya pauni milioni 35 zilizokataliwa na kocha Brendan Rodgers,
aliyesisitiza kuwa hayuko tayari kumuuza mtikisa mabao wake huyo mwenye umri wa
miaka 30 chini ya dau la pauni mil. 55.
Tayari Gunners
ilishakubali kumlipa Suarez mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki kumng’oa mkali
huyo Anfield.
Suarez, hata hivyo,
anadaiwa kupendelea kutua Madrid kuliko Arsenal, akiwa na nia ya kukimbia
jinamizi la matukio tata dimbani katika soka la England.
Na sasa Madrid
inamthaminisha Higuain kwa dau la pauni milioni 35 baada ya kupokea ofa ya
thamani hiyo kutoka Napoli, ambapo inajiona iko sahihi kuongeza dau la pauni milioni
20 kukamilisha kitita cha pauni milioni 55 zinazotakiwa na Rodgers.
No comments:
Post a Comment