Wewe ndio mchizi wetu |
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, jana
aligeuka shujaa kwenye mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika Bwalo la Maofisa
wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya wanachama
wapatao 700.
Tofauti na dalili za awali pengine mkutano huo ungekewa na
presha kubwa ya wanachama kuhoji mambo mbalimbali ya kiuongozi, mkutano huo
jana uligeuka shangwe na nderemo za wanachama kiasi cha kubariki kila
walichoelezwa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mkutano huo, wanachama
wengi walionesha kuridhishwa na utendaji mzima wa kiongozi wao licha ya kuwepo
changamoto mbali mbali pia wanastahili kuupongeza uongozi uliopo madarakani
chini ya Rage.Baadhi ya wanachama wameomba mabadiliko mbali mbali katika
utendaji wa klabu wakiamini klabu hiyo chini ya Rage, watapata mafanikio
makubwa katika msimu ujao.Jambo jingine ni wanachama kuombwa kuzika tofauti
zilizojitokeza hadi kuibua mgogoro ndani ya klabu hiyo kiasi cha viongozi
kujikuta wakigongana wao kwa wao hivyo timu kushindwa kufanya vizuri.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Rage alisema hatarajii
mapinduzi katika uongozi wake kwani wamekuwa wakichapa kazi kwa mujibu wa
katiba ya klabu hiyo, hivyo msimu ujao
utakuwa ni wa mafanikio kwa klabu hiyo.
“Naaamini mambo yatakwenda vizri katika msimu ujao wa ligi
na timu itafanya vizuri kutokana na mipango na mikakati tuliyojiwekeza,”
alisema Rage na kuongeza wataitisha mkutano mwingine kabla ya Novemba na
kuongeza:
“Tunataka tuwe na sera bora za utawala na utendaji ambapo
kupitia sera hizi kutakuwa na mfumo bora wa utendaji, kiutawala, kimajukumu na
kiuwajibikaji ambapo kila mtu atajikuta anafanya kazi yake,” alisema Rage.
Rage pia amesisitiza msimamo wa kulifuta tawi la Mpira Pesa
kwa hoja wanachama wa tawi hilo wamekuwa
wakienda kinyume na taratibu za klabu hiyo wakitaka kuwa juu ya uongozi na
kusema jambo hilo halikubaliki kamwe.
“Mpira pesa hawako juu ya Klabu ya Simba, bali ndani ya
klabu hiyo, hivyo hatuwezi kuvumilia kuona wanataka kukaa juu ya klabu kitaifa,
suala ambalo ni kinyume na utaratibu kabisa,” alisema Rage.
Rage alibainisha kuwa uongozi uliopo madarakani utaendelea
kuwajibika katika mambo yote licha ya wanachama hao kutaka kujua hatima ya
nafasi ya Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akisema nafasi hiyo
imezibwa na Joseph Itang’are ‘Kinesi.’
Katika mkutano huo ulidumu kwa dakika 60, agenda zilikuwa
kuthibitisha kumbukumbu ya mkutano uliopita, hotuba ya Mwenyekiti na kupokea na
kujadili taarifa za kazi kutoka kamati ya utendaji.
Nyingine ni kudhibitisha hesabu za fedha zilizokagaliwa za
mwaka uliotangulia, kuthibitisha taarifa za chombo cha ukaguzi na hatua
zilizochukuliwa na vyombo
vya utendaji na kudhibitisha bajeti kwa mwaka ujao.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huo majira ya saa 5 asubuhi,
ndipo ukumbi ukagubikwa na shangwe za wanachama wakiupngeza uongozi wa klabu
hiyo
hadi kumbeba Ragea akionekana ni shujaa.
Hitimisho hilo lilikwenda sambamba na wanachama
waliohudhuria mkutano huo, kupewa tiketi ya kuingilia uwanja wa Taifa kujionea
mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Simba na URA ya Uganda.
Kuelekea mkutano huo, baadhi ya wanachama walikuwa wakihoji
uhalali wa mkutano huo wakidai umeitishwa kinyume cha katiba na wakapanga
kwenda mkutanoni kuung’oa.
No comments:
Post a Comment