Gerardo Martino ‘Tata’ |
Gerardo kumrithi
Vilanova
KOCHA wa zamani wa timu
ya taifa ya Paraguay, Gerardo Martino
‘Tata’ anapewa nafasi kubwa ya kuziba nafasi ya Tito Vilanova, aliyejiweka
kando kutokana na sababu za kiafya.
Vilanova (44),
aliyekuwa ametwa nafasi hiyo baada ya kuondoka kwa Pep Guardiola, amekuwa
akisumbuliwa na kansa ya koo kwa muda mrefu.
Kuna habari kuwa,
Martino mwenye umri wa miaka 50, alitarajiwa kwenda nchini Hispania kwa
mazungumzo ya kazi hiyo.
Martino, aliyeipa
Newell's Old Boys ubingwa wa Argentina msimu uliopita, kwa sasa yupo nje ya
mkataba na wakali hao.
Ni kocha mwenye
rekodi ya kubeba ubingwa wa Paraguay na mwaka 2007, alitwaa tuzo ya Kocha Bora
Amerika Kusini.
Kocha huyo
aliyezaliwa Novemba 20, 1992, pia amewahi kufundisha Brown de Arrecifes,
Platense, Instituto, Libertad, Cerro Porteño, Colón, Libertad na timu ya taifa
ya Paraguay kuanzia 2006 hadi 2011.
No comments:
Post a Comment