Manchester Utd kumsajili Benteke Januari
KLABU ya Manchester United imeonesha nia ya kumtaka mchezaji wa Aston Villa, Christian Benteke.
David Moyes amekuwa shabiki mkubwa wa mchezaji huyo katika Ligi Kuu England ambaye anaamini anaweza kuziba pengo la Wayne Rooney kama hatoweza kuongeza mkataba mpya.
Moyes amemtengea mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, mshahara wa Pauni 60,000 kwa wiki.
Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert amesema hatokuwa na uweza wa kumzua mshambuliaji huyo kutimka kwa kuwa ofa hiyo ya mshahara ni kubwa kwake.
Moyes pia ameonesha nia ya kumuhitaji mwengine mshambuliaji Edinson Cavani anayekipiga Paris Saint-Germain.
Benteke ndiyo tarajio lao kubwa katika usajili wa dirisha dogo la Januari.
No comments:
Post a Comment