Saturday, September 7, 2013

Ozil aliimezea mate Man Utd

Mesut Ozil aliimezea mate Man Utd
WAKATI Mesut Ozil akitua Arsenal dakika za majeruhi kwa kitita cha pauni mil 42.5, wataalamu wa masuala ya soka wanasema kiu ya nyota huyo wa Kijerumaini, ilikuwa ni kujiunga na Manchester United.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, Graham Hunter, alisema Jumatatu iliyopita kuwa licha ya kutua Emirates, lakini alikuwa akiwindwa pia na Man Utd chini ya kocha wake David Moyes.
Licha ya United kukana kuwahi kuwa na mpango huo, Hunter akizungumza na Sky Sports, alisema anaamini kuondoka kwa Ozil Real Madrid kulipigwa presha na ujio wa Gareth Bale, wakati huo akiisubiri kwa hamu ofa ya kwenda Old Trafford ambayo haikufanikiwa.
"Ozil na baba yake wote walitamani aende Old Trafford, waliona Old Trafford ni mahali pazuri kisoka,” alisema.

No comments:

Post a Comment