Yanga SC yashikwa, Mnyama aua
Abdi Banda kati kati akiwatoka wachezaji wa Yanga. |
Jerry Santo akipiga penati iliyozaa goli dakika ya 90. |
MABINGWA watetezi
wa Lgi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC jana walilazimishwa sare ya bao 1-1 na
Coastal Union ya Tanga katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
Salaam.
Yanga walipata bao dakika ya 68, na Mshambuliaji wao hatari
Didier Kavumbagu baada ya kupokea krosi safi iliyopigwa na David Luhende.
Hivyo, Coastal Union walisawazisha dakika ya 90 kwa mkwaju
wa penalti iliyofungwa na Jerry Santo, baada ya Luhende kuunawa mpira ndani ya
kumi na nane.
Hivyo kila timu ikanyakua pointi moja, na kufikisha pointi
nne kila mmoja katika.
Baada ya mechi kumalizika, polisi waliamua kuwatawanya
mashabiki wa Yanga kwa kutumia mabomu ya machozi, kutokana na kufanya fujo kwa
kukerwa na uchezeshaji wa mwamuzi.
Wale watani wao wa Jadi, Simba ilipata ushindi mwembamba wa
bao 1-0 kutoka kwa JKT Oljoro.
Nayo Ashanti United jana imeendelea kuwa mdebwedo baada ya
kuchapwa bao 1-0 na JKT Mgambo.
Bao pekee la Mgambo JKT walioanza ligi hiyo kwa kichapo
kutoka kwa JKT Ruvu, lilifungwa dakika ya 62 na mtokea benchi, Fully Maganga.
Ni kipigo cha pili vijana hao wa Ilalala, Dar es Salaam
wakitoka kulimwa mabao 5-1 na mabingwa watetezi, Yanga.
Matokeo mengine
Mbeya City 2-1 Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar 1-0 Kagera Sugar
Azam 2-0 Ryno Rengers
JKT Ruvu 3-0 Prisons
JKT Ruvu 3-0 Prisons
No comments:
Post a Comment