Tuesday, August 27, 2013

Mourinho ampa Wayne Rooney saa 48 kuamua

Mourinho ampa Rooney saa 48 kuamua
 
 
 
MRENO Jose Mourinho amempa Wayne Rooney muda wa saa 48 awe ametoa jibu ramsi kama atahama Old Trafford na kwenda Stamford Bridge ama vipi.
Mourinho ameamua hivyo, licha ya kocha wa Man Utd, David Moyes kuwahi kutamka bayana kuwa hayuko tayari kumtoa nyota huyo kwa bei yoyote.
Aidha, Mourinho amesisitiza hilo siku moja tu tangu timu hizo zivune sare ya bila kufungana katika mechi ya Ligi Kuu, ikiwa ya pili kwa kila timu tangu kuanza kwa ligi hiyo Agosti 17.
Hayo yote kutokana na Rooney kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mechi hiyo.
Aidha, Mourinho amemwaga sumu hiyo wakati ambao Rooney (27), akionesha wazi kuwa
anataka kuondoka kutokana na mazingira halisi ya Old Trafford kwa sasa juu ya nafasi yake kwenye kikosi chini ya Moyes.
"Kwa namna moja au nyingine, aseme kama anataka kubaki au kuondoka," alisema Mourinho aliyerejea Stamford Bridge msimu huu akitokea Santiago Bernabeu.
Tangu Rooney atue Old Trafford mwaka 2002 akitokea Everton, ameifungia Manchester United jumla ya mabao 156, hivyo kuwa miongoni mwa nyota muhimu katika safu ya ushambuliaji.
Alipoulizwa kuhusu nyota wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto’o wa klabu ya Anzhi Makhachkala, alisema hilo pia litajulikana baada ya masaa 48.
"Kwa kocha kama mimi, klabu kama Chelsea na watu wafanyai kazi pamoja nami, hatutaki kupoteza muda kwa mchezaji wa klabu asiyotaka kumuuza,” alisema Mourinho aliyewahi kuipa Chelsea ubingwa wa Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment