Monday, August 26, 2013

KUELEKEA MECHI YA MAN UTD NA CHELSEA LEO Moyes na Mourinho waogopana

KUELEKEA MECHI YA MAN UTD NA CHELSEA LEO
Moyes na Mourinho waogopana
KLABU za Manchesater United na Chelsea zimejikuta katika wakati mgumu kutokana na kila moja kujikuta ikihakikisha inafanya kila liwezalo kukwepa kupokea kipigo kutoka kwa mwenzake.
Klabu hizo ambazo zinatarajiwa kukutana leo katika mchezo wa ligi kuu huku United ikiwa na historia ya kushinda mara mbili na Chelsea mara tatu hali inayoonesha kwamba kila moja ina nafasi ya kushinda mchezo huo lakini kama leo mmoja wao atafanikiwa kuichapa nyingine atakuwa ameandika historia isiyosahaulika.
Iwapo Chelsea watakubali kupokea kipigo kutoka kwa United, itawapa wakati mgumu katika mchezo wao wa Super cup utakao wakutanisha na wababe kutoka Ujerumani klabu ya Bayern Munich.
Mshindi wa mchezo huo kati ya klabu ya Man Utd na Chelsea utachangia kuiwezesha klabu husika kuitangaza na kuiweka katika nafasi nzuri kwenye msimu huu mpya wa Ligi Kuu England.
Kwa upande wa David Moyes anatakiwa kushindwa mechi hii kutokana na ukweli kwamba ni kocha mpya kukutana na Chelsea akiwa na Man United, kwani kwake ushindi ndicho kitu anachokihitaji huku akikwepa pia kupokea kipigo kutoka kwa Chelsea.
Mchezo huo unaonekana kujaa na msisimko kutokana na kwamba wakati Moyes alipokuwa kocha wa Everton klabu ya Chelsea imewahi kumchakaza, hivyo anahitaji kujenga heshima mpya ndani ya Old Trafford.
Klabu zote zinaonesha kujiimarisha katika ushambuliaji na ukuta usiopitika kirahisi hivyo mechi hiyo inategemewa kuwa kali na nzuri!

No comments:

Post a Comment