KLABU ya Real Madrid na Tottenham zimeafikiana juu ya nyota wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale aende Santiago Bernaneu kwa kitita cha euro mil 100.
Kiasi hicho kinazidi kile kilichotolewa na klabu hiyo mwaka 2009 kwa Cristiano Ronaldo kumng’oa Old Trafford kwa euro mil 93.
Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy, alisema juzi mpango huo umefanikiwa baada ya majadiliano ya kina baina ya klabu hizo mbili.
Japo Real Madrid ilikuwa bado haijapata uhakika wa nyota huyo, Alhamisi iliyopita mashabiki wa Santiago Bernabeu walikuwa na fulana zenye jina la Bale na11.
Kuna habari kuwa, tayari klabu hiyo imeanza kujenga jukwaa rasmi ambalo litatumika kwa utambulisho wa mchezaji huyo kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Habari zinasema licha ya klabu hiyo kufanya maandalizi ya utambulisho wa Bale, yaelezwa presha yake haiwezi kulinganishwa na yale ya Cristiano Ronaldo, Kaka au Karim Benzema.
No comments:
Post a Comment