Simba yanasa mshambuliaji,
Joseph Owino amwaga wino
Mshambuliaji Mpya wa Simba, Betram Mombeki (kulia) akimwaga wino |
KATIKA kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa
Ligi Kuu soka Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 24, klabu ya Simba imemsajili
rasmi beki wa kati, Joseph Owino na mshambuliaji wa zamani wa Pamba FC ya
Mwanza, Betram Mombeki.
Mombeki aliyekuwa akiishi na kucheza soka nchini Marekani,
alisaini jana mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo yenye maskani
yake mitaa ya Msimbazi.
Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya uongozi wa Simba,
wameamua kumsajili Mombeki baada ya kuridhishwa na kiwango alichokionesha
wakati wa majaribio yake.
Kiongozi huyo alisema wanaamini hawajafanya makosa kumsajili
wingi huyo ambaye ameonesha kiwango cha juu kipindi chote tangu ajiunge na
klabu hiyo kwa majaribio hivyo atawasaidia katika michuano mbalimbali.
Kusajiliwa kwa Mombeki kunafanya idadi ya wachezaji wazawa
waliosajiliwa Simba kufikia watano ambapo awali iliwanyakua mshambuliaji Zahor
Iddi Pazi aliyekuwa akicheza kwa mkopo JKY Ruvu kutoka Azam, kipa Andrew Ntala
kutoka Kagera Sugar na beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Mtibwa Sugar na
Twaha Shekuwe ‘Messi’ wa Coastal Union.
No comments:
Post a Comment