Beckham kumiliki timu Marekani
Beckham (kulia) akiwa pamoja na Ronaldo walipokutana jijini, Los Angeles, Marekani |
NYOTA wa zamani wa Los Angeles Galaxy ya Ligi Kuu ya
Marekani, David Beckham, anakaribia kutangazwa kuwa mmiliki na bosi mpya wa
klabu jijini Miami.
Becks, 38, ana chaguo linalomruhusu kununua hisa katika timu
ya Ligi Kuu ya Marekani ‘Major League Soccer – MLS’ baada ya kuichezea LA
Galaxy na sasa yuko katika nafasi ya kutumia nafasi hiyo.
Mkataba wa Beckham na Galaxy ulikuwa na kipengele
kinachomuwezesha nyota huyo kuanzisha ama kumiliki klabu katika Ligi Kuu kwa
dau linaloanzia dola za Marekani milioni 25.
Beckham ameripotiwa mara kadhaa kukutana na bilionea raia wa
Bolivia, Marcelo Claure, ambaye amedhamiria kuamua na nyota huyo wa zamani wa
Man United na Real Madrid, kuhusu uanzishwaji wa timu mpya na uwanja mpya.
Mkuu wa MLS, Don Garber, alisema: “Sisi tunadhani itakuwa
kali David Beckham kushiriki katika ligi yetu. Tutaendelea kujadiliana naye kwa
uhakika kuhusu hilo.”
Beckham alistaafu kuichezea LA Galaxy baada ya kumalizika
kwa msimu uliopita, alioiwezesha kuipa klabu hiyo ubingwa wa Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment