Luiz kuing'arimu Bayern pauni mil. 60
MABINGWA wa Europa League, Chelsea, wamewatunishia misuli
mabingwa wa Ulaya Bayern Munich na kuwaambia kuwa kiungo Mbrazil inayemuwinda,
David Luiz, atawagharimu pauni milioni 60.
Kocha mpya wa Bayern, Pep Guardiola, amebainisha nia ya kumuwania
Luiz, 26, ili kukipa nguvu kikosi chake, huku akitenga kitita cha pauni milioni
40 kumng’oa nyota huyo Stamford Bridge na kumpeleka Allianz Arena.
Lakini Chelsea chini ya Kocha mpya, Jose Mourinho,
imesisitiza kuwa haiko tayari kumuuza Luiz na The Bavarians aidha ikubali kutoa
pauni milioni 60 au iachane na jaribio la kumsajili nyota huyo.
Bayern ilijiona iko katika njia sahihi kufikia utimilifu wa
uhamisho wa Luiz, ambaye aliigharimu Chelsea kitita cha pauni milioni 21.3
ilipomsajili akitokea Benfica ya Ureno, Januari 2011 kabla ya dili lao
kupingwa na The Blues.
Nguvu ya Bayern pia ilitokana na madai yaliyofunika ujio wa
Mourinho, ambaye alidaiwa kutokuwa na mipango ya muda mrefu na Mbrazil huyo,
ambaye alikuwa mhimili wa Chelsea kutwaa mataji mawili ya Mabingwa Ulaya na
Europa League.
No comments:
Post a Comment