Newcastle yanawa mikono kwa Gomis
Bafetimbi Gomis |
TIMU ya soka inayoshiriki Ligi Kuu England imejitoa katika
mbio zake za kumsajili mshambuliaji raia wa Ufaransa anayeichezea klabu ya
Lyon, Bafetimbi Gomis.
Loic Remy |
Hata hivyo upande wa Klabu yake ya Lyon waliikata ofa hiyo wakitaka
waongezwe.
Kocha wa Newcastle, Alan Pardew amekuwa na hamu ya kuongezea
makali katika safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili Gomis ambaye alifunga mabao 18
katika msimu ulioisha kwa Lyon.
Kwa sasa ameelekeza nguvu yake yakutamani kumsajili
mshambuliaji wa QPR Loic Remy kwa mkopo wa
muda mrefu.
Japokuwa anasafu kali ya ushambuliaji inayoongozwa na
Waafrika, Shola Ameobi na Papiss Cisse lakini Pardew na uongozi wa klabu yake wanafanya
kazi ya kuhakikisha wanaleta sura mpya kwenye klabu hiyo
No comments:
Post a Comment