Yanga yatoa walaka kwa Azam Tv
Rais wa Yanga akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) |
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
Hivi karibuni, Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi
yampito Bodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa
kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3
(mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football
Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television,
Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:
1. BODI YA TPL
1.1 Bodi iliyoko
sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa
kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe
……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi
wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL
iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL
iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2. UTARATIBU WA
DUNIA NZIMA
2.1 Haijawahi kutokea
katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana
katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha
habari cha Klabu ya upinzani.
2.2 Mfumo
(undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa
YANGA iachie urushwaji wa michezo yake
ya soka yarushwe na Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika
soka ya Tanzania.
2.3 Makubaliano
kati ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasema kwamba Klabu
ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa
michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote
kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya
timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.
2.4 Kamati ya
Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao
hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi,
lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:
2.4.1 Vilabu vya
mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi;
2.4.2 Vilabu vya
mpira vinavyoendeshwa na Wanachama;
2.4.3 Vilabu vya
mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.
3. MIGOGORO YA
MASLAHI
3.1 Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya
Azam na kwa hivyo mazungumzo ya siri
kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.
3.2 Makampuni ya
Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa
vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu zaidi
kuliko mprira wa miguu, kama vile Azam
F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo
kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu
inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.
3.3 Azam na YANGA
wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA,
Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika
kwa matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake
n.k.
4. KUTOKUWA NA
UWAZI
4.1 Mkataba wa
utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao bado
haujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya
habari, na vyombo ambayo wako tayari
kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha
mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu
(Tanzania Premier League).
4.2 Ukosefu wa
uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL
haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya
ombi hilo kwaTPL.
5. MAZINGATIO
YA KIBIASHARA
5.1 Mamlaka ya
kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania
Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL
inasingizia kwamba leseni ya matangazo
ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa
kuukubali "lock, stock and barrel."
5.2 TPL inaelezea
kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji
wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama
"makubaliano ya udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo
sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara
inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo
wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.
Kwa mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni
mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo
urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya
YANGA Dar es Salaam huingiza makusanyo
ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25%
katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya
mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa
kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata
siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa,
wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji) walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja
kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati ya Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano
yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu
yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo,
Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam
Television.
Msisitizo wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani
michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na
Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam
Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa
Vodacom Premier League katika Azam Television.
......................
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013
No comments:
Post a Comment