Naser Chadli |
Spurs yanasa saini ya Chadli
KLABU ya Tottenham imethibitisha kumsajili nyota wa
kimataifa wa Ubelgiji, Naser Chadli kutoka klabu ya FC Twente kwa ajili ya msimu ujao.
Winga huyo mweye umri wa miaka 23, tayari jana alikuwa mjini
hapa kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu hiyo akifuata nyayo Wabelgiji
wenzake, Mousa Dembele na Jan Vertonghen.
Chadli, anayecheza pia kama winga wa pembeni, ni mchezaji wa
pili kusajiliwa Spurs akitanguliwa na
Mbrazil, Paulinho kutoka Corinthians aliyegharimu kiasi cha pauni mil
20.
Baada ya kukamilisha taratibu zote, ataungana na kikosi cha
Kocha Andre Villas-Boas kilichopo Hong Kong kujiandaa na msimu mpya.
No comments:
Post a Comment