Sunday, July 21, 2013

Reina na Benitez
Kipa Reina amfuata Benitez kwa mkopo
KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kipa wa timu hiyo, Pepe Reina, atakwenda kwa mkopo katika klabu ya Napoli kutokana na sababu za kiuchumi.
Mipango hiyo inatokana na Napoli kutokuwa na uhakika wa kipa wake Julio Cesar ambaye hadi sasa hajaamua kuongeza mkataba.
Rodgers amesema Reina ataondoka Anfield msimu huu kwani Liverpool hawana uwezo wa kumlipa baada ya kutumia euro mil 10 kumsajili Simon Mignolet kutoka Sunderland, Juni mwaka huu.
Reina, aliyebakisha mkataba wa miaka mitatu ya kuicheza Liverpool, amekuwa akilipwa mshahara wa euro  128,000 kwa wiki, akiwa Napoli, atakuwa chini ya Rafa Benitez.
Benitez tayari amesajili nyota kadhaa kama kipa Rafael kutoka Santos kwa euro mil 5, lakini amekuwa akimhitaji Reina kuongeza ushindani wa namba.

No comments:

Post a Comment