Jupp Heynckes |
Heynckes agoma kumrithi Vilanova
KOCHA Jupp Heynckes (68) aliyempisha Pep Guardiola katika
timu ya Bayern Munich baada ya kuipa mataji matatu msimu uliopita, amekataa
kujiunga na Barcelona ya Hispania.
Ingawa amekuwa akitajwa katika orodha ya makocha wanaopewa
nafasi ya kuinoa Barcelona, Heynckes amesema hana mpango wa kufundisha soka kwa
sasa.
Alisema licha ya Barcelona kuondokewa na kocha wake Tito
Vilanova ambaye amejiweka kando kwa matatizo ya kiafya, kocha huyo amesema
anataka kufaidi matunda ya kazi aliyofanya kabla ya kustaafu.
Heynckes mwenye rekodi ya mafanikio makubwa katika
ufundishaji wake, msimu uliopita ameiwezesha Bayern kutwaa mataji matatu.
Mataji hayo ni ubingwa wa Bundesliga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Ligi.
Aidha, Heynckes amekuwa ni mwenye rekodi bora na michuano ya kimtaifa kwani
mwaka 1998, aliipa Real Madrid ubingwa wa Ulaya.
“Nimekuwa ‘bize’ kwa muda mrefu, lakini sasa nimeamua
kufanya kazi nyingine ya ufugaji na kutunza bustani, hivyo itakuwa vigumu kwangu
kurejea kufundisha bada ya kuondoka Bayern Munich,” alisema alipozunguza na Sky
Sport News na kuongeza:
“Natambua hisia za
mwili wangu ambao mara nyingi umekuwa ukitamani kufundisha soka, lakini ni
wakati sasa wa kubudika na matunda ya kazi niliyofanya kwa miaka mingi.
Hneyckes alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa kama yu tayari
kuziba nafasi ya Vilanova ingawa baadhi ya makocha wamekuwa wakitajwa kama
Gerardo Martino.
Kuna habari kuwa, Gerardo ndio chaguo la Lionel Messi, japo
kuna majina mengine yanataja kwama Luis Enrique wa klabu ya Celta Vigo.
Enrique, 43, amekuwa mwenye mafanikio makubwa katika miaka
mitatu hivi akiwa na kikosi cha pili cha Barcelona tangu mwaka 2008 na 2011
kabla ya kwenda AS Roma ambako hakupata mafanikio.
No comments:
Post a Comment