Mourinho: Wenger ni mchizi wangu
MAKOCHA
wa klabu hasimu za Arsenal na Chelsea, Arsene Wenger na Jose Mourinho, kwa sasa
ni kama maswahiba wakubwa, ambapo Mourinho amekiri kuwa anamheshimu mno Wenger
licha ya klabu zao kuwa pinzani.
Ukaribu
wa Wenger na Mourinho, umeonekana kwa wawili hao kuambatana pamoja wakati wa
chakula cha usiku nje ya makazi yao, ambapo Special One amesisitiza kuwa
heshima yake kwa Wenger inatokana na mafanikio yaliyotukuka akiwa Arsenal.
Mourinho
raia wa Ureno, alisema: “Yeye ni mtu mzuri sana. Namheshimu sana yeye na daima
natarajia kuonyesha heshima zaidi kwake.
“Nisingependa
kuwa na tatizo lolote baina yetu. Wakati unapokuwa huko katika ligi hiyo na
wakati kunapokuwa hakuna mechi baina yetu, ni rahisi mno kuwajua watu.
“Na
mimi nilikuwa na nafasi bora zaidi ya kukutana na yeye wakati nilipoondoka
England, katika UEFA, michuano ya Euro, Kombe la Dunia. Tulikutana katika chakula
cha jioni na ilikuwa ni nyakati nzuri. Nilikuwa nafurahia kuzungumzia soka na
yeye.”
Mourinho
alienda mbali zaidi na kufichua kuwa yeye anaweza kujifunza kutoka kwa Wenger,
namna sahihi ya kudumu na klabu moja kwa zaidi ya miaka mitatu.
Mreno
huyo alisema: “Wenger ananifundisha mimi namna gani ya kudumu hapa kwa miaka
17. Hilo lilikuwa moja agenda wakati wa mazungumzo yetu ya mwisho.
“Kupewa
na kupata heshima kama anayopata kutoka kwa bodi ya klabu ni jambo muhimu. Sio
kutokana na uso wake nzuri, bali ni kutokana na kazi bomba aliyofanya.
“Alikuwa na nafasi nyingi tu za kutimka Gunners, yote ni kutokana na nia nzuri ya klabu kwake, hivyo wakati akikataa ofa za kuhama na kutaka kubaki Emirates ni kwa sababu anapapenda na sababu ikiwa ni matarajio yake ya baadaye,” alimaliza Mourinho.
“Alikuwa na nafasi nyingi tu za kutimka Gunners, yote ni kutokana na nia nzuri ya klabu kwake, hivyo wakati akikataa ofa za kuhama na kutaka kubaki Emirates ni kwa sababu anapapenda na sababu ikiwa ni matarajio yake ya baadaye,” alimaliza Mourinho.
No comments:
Post a Comment