Madrid yamvalia njuga Bale
Gareth Bale |
MIAMBA
ya soka la hapa, Real Madrid, juzi usiku ilipiga hatua inayotajwa kuweza kuwa
ya mwisho katika jitihada zake za kupata saini ya winga Gareth Bale wa
Tottenham kwa ofa inayofikia thamani ya pauni milioni 95 ikihusisha pesa na
wachezaji wawili.
Madrid
imeripotiwa kuwa iko tayari kutoa kitita cha pauni milioni 51, sambamba na
wachezaji wawili, Angel Di Maria anayethaminishwa kwa dau la pauni milioni 25
na Fabio Coentrao pauni milioni 19 – kufanikisha ililoliita ‘dili la karne.’
Tayari
Madrid ilishatoa ofa rekodi ya dunia ya pauni milioni 81 kuomba ridhaa ya
kumnasa winga huyo wa kimataifa wa Wales, ambalo lilikataliwa na Spurs na
kumshangaza hata mchezaji husika.
Lakini,
Rais wa Madrid, Florentino Perez, ameenda mbali zaidi katika ofa mpya ya
kujaribu kumfanya Bale kuwa nyota mpya wa The Galactico.
Ofa
hii mpya ya Madrid, inatabiriwa kumsukuma Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy,
ambaye amekuwa mbali, asiyetaka kujadili suala hilo, kuridhia uhamisho huo.
Bale
juzi alipaza sauti kumwambia Levy kuwa anahitaji ridhaa ya kwenda kujiunga
Madrid, huku akimkumbusha mwenyekiti huyo kukumbuka ahadi kuwa angemruhusu
kuhama kama klabu hiyo ya White Hart Lane ingekosa tiketi ya mabingwa Ulaya.
Licha
ya kumuomba mwenyekiti kubariki uhamisho wake, Bale, 24, amekana mbinu chafu ya
kuishinikiza Spurs kumuuza.
Kocha
wa Tottenham, Andre Villas-Boas, anatambulika alivyo shabiki wa winga wa
kimataifa wa Argentina, Di Maria, 25 ambaye anaambatanishwa katika jaribio la
sasa la Madrid.
Na haitarajiwi kama anaweza
kukana kuungana na Mreno mwenzake Coentrao, 25, ambaye anaweza kutumika kama
beki/winga wa kushoto - mzalishaji wa mashambulizi ya pembeni kutokea nyuma.
No comments:
Post a Comment