Mkenya azimia kwenye mbio
Irine Chebet Cheptai |
MKIMBIAJI wa mbio ndefu wa kimataifa wa Kenya , Irine
Chebet Cheptai, juzi alikimbizwa hospitali kwa matibabu baada ya kupatwa na
mshituko wa moyo kwenye Uwanja wa Olimpiki baada ya kumaliza mbio za mita
3,000.
Cheptai, binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa
nafasi ya 11, katika muda bora zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia
dakika 8:56.20, lakini akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka
mstari wa kumalizia.
Madaktari waliokuwa uwanjani hapo wakaharakisha
kumtundikia mtungi wa Oksijeni, ambapo kwa mujibu wa taarifa kuhusiana na tukio
hilo zilipasha
kuwa alikuja kurejewa na fahamu akiwa hospitalini.
Tukio lake limeshtua wengi kutokana na kukimbia
katika mbio fupi kulinganisha na zile alizozoea za mita 5,000, ambazo
ameshiriki Diamond League mara mbili msimu huu, na anakumbukwa kwa rekodi yake
ya dakika 14:50.99 jijini Shanghai, Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment