Ahly, Zamalek zatoka sare 1-1
KIUNGO Mohamed Aboutrika wa
Ahly, Jumatano usiku aliifungia bao timu yake kwa mkwaju wa penalti na
kuisaidia kuvuna sare ya bao 1-1 dhidi ya Zamalek katika mechi ya kwanza ya
Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa mjini hapa.
Ingawa baadhi ya mechi za
makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho zilichezwa
mwishoni mwa wiki, mechi ya timu hizo mbili ilisogezwa hadi Jumatano kutokana
na vurugu zilizoukumba mji wa Cairo na Alexandria .
Aboutreika alifunga bao kwa
penalti dakika 27 kabla ya filimbi ya mwisho baada ya Salah Soliman wa Zamalek
kumchezea vibaya mshambuliaji Ahmed Abdel-Zaher.
Bao hilo
lilirejesha furaha kubwa wapenzi na mashabiki wa Ahly kutokana na timu yao kuwa nyuma tangu
dakika ya nane baada ya Ahmed Gaafar kuifungia timu yake bao, akimtungua kipa Sherif
Ekramy.
Kwa sare hiyo, timu zote za
kundi A, zimelingana kwa pointi moja kwani katika mechi ya mwishoni mwa wiki,
timu za Orlando
Pirates ya Afrika Kusini na AC Leopards ya DR Congo zilishindwa kufungana.
Mechi hiyo ya Zamalek na
Ahly, ilichezwa mjini El Gouna, badala ya Cairo
kutokana na sababu za kiusalama baada ya uwepo wa maandamano ya wafuasi wa
aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Morsi.
Ingawa awali mechi hiyo
ilitakiwa ipigwe bila mashabiki, lakini kutokana na ulinzi mkali wa vyombo vya
usalama, mashabiki wapatao 7,000 waliingia kwenye uwanja wenye uwezo wa kubeba
watu 12,000.
Matokeo hayo yanaifanya Ahly
kuongoza kundi A, ikiwa na pointi moja ikifuatiwa na wapinzani wakubwa katika ligi
ya Misri, Zamalek pia wenye poiinti moja kama
ilivyo kwa Leopards ya DR Congo na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Libolo FC ya Angola inaongoza kundi B, ikiwa na pointi moja
ikifuatiwa na Coton Sport ya Cameroon ,
Sewe ambazo hazijacheza na Esperance ya Tunisia
iliyopoteza mechi ya kwanza mjini Luanda .
No comments:
Post a Comment