Dortmund yamkaribisha rasmi Guardiola
PEP
Guardiola juzi usiku alijikuta akiandika historia ya kuchapwa katika mechi ya
kwanza ya kimashindano klabuni Allianz Arena, baada ya kupokea kipigo cha mabao
4-2 kutoka kwa Borussia Dortmund na kutwaa ubingwa wa Supercup.
Bayern
Munich, ambayo iliichapa Dortmund katika fainali ya Mabingwa Ulaya Mei mwaka
huu kwenye dimba la Wembley jijini London, ilishindwa kumzuia Marco Reus
kufunga mara mbili na kuipa Dortmund ubingwa ndani ya Uwanja wa
Westfalenstadion.
Wakati
Bayern ikishindwa kurejea ilichofanya katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,
Mholanzi Arjen Robben – ambaye alifunga bao la ushindi Wembley, alimudu kurejea
hilo kwa kufunga mabao yote mawili juzi.
Akizungumzia
pambano hilo baada ya filimbi ya mwisho, Guardiola alisema: "Ingawa
tumepoteza pambano hili, bado sihisi kuwa Dortmund walikuwa bora kuliko sisi.
"Tuna
siku 10 kabla ya ufunguzi wa msimu wa Bundesliga, hivyo tuna muda wa
kusahihisha makosa madogo madogo yaliyotugharimu katika mechi hii,"
aliongeza Guardiola.
Guardiola,
ambaye alitwaa jumla ya mataji 13 katika miaka yake minne ya kuinoa FC
Barcelona aliyoiacha mwaka jana, ana kibarua kigumu kudumisha makali
yaliyoachwa na kocha aliyechukua nafasi yake Jupp Heynckes klabuni hapo.
Chini
ya Heynckes, Bayern iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Ujerumani kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu ‘Bundesliga,’ Mabingwa Ulaya na Kombe la Ujeruman (DFP
Pokal), iliyotwaa msimu uliopita.
Bayern
ambayo ilicheza bila nyota wake Franck Ribery na Bastian Schweinsteiger, huku
ikimkosa pia Mario Gotze – aliyetua hapo akitokea Dortmund, hiki ni kipigo
chake cha kwanza wakati huu wa maandalizi kuelekea msimu mpya.
Kabla
ya hapo, Bayern ilizichapa Fanclub Wildenau mabao 15-1, TSV Regen 9-1, Paulaner
Dream Team 13-0, Brescia 3-0, Sonnehof Grossapac 6-0, Hansa Rostock 4-0,
Hamburg 4-0, Borussia Monchengladbach 5-1, kabla ya kuichapa Barcelona mabao
2-0.
Kwa
upande wake kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp alisema: "Ilikuwa ni mechi
kubwa, timu zote zikipanda kushambulia na kujilinda vema, kana kwamba hakuna
kesho.
“Jambo
la msingi ni kuwa Bayern sio wapinzani wetu pekee, tumejibidisha kama sisi.”
Bayern inatarajia kufungua msimu wa Bundesliga kwa kuwavaa Borussia Monchengladbach Ijumaa ya Agosti 9, wakati Dortmund itaumana na Augsburg siku baadaye.
Bayern inatarajia kufungua msimu wa Bundesliga kwa kuwavaa Borussia Monchengladbach Ijumaa ya Agosti 9, wakati Dortmund itaumana na Augsburg siku baadaye.
No comments:
Post a Comment