Kashfa ya dawa inakera - Usain Bolt
BINGWA mara sita wa Olimpiki,
Usain Bolt wa Jamaica ,
amesema anakabiliwa na jukumu zito la kuurejeshea heshima mchezo huo kitaifa na
kimataifa baada ya nyota wenzake kuingia kwenye tuhuma za kutumia dawa za
kusisimua misuli miezi miwili iliyopita.
Kauli hiyo imekuja huku
wachezaji mahiri wa mbio fupi,
Asafa Powell wa Jamaica
na Tyson Gay ambao wameangukia kwenye tuhuma hizo wakiungana na Sherone Simpson
ndani ya mwaka huu.
Bolt (26), aliyeshiriki mbio
za hisani wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Olympic, alisema ni jukumu lake na
wachezaji wengine kufanya kweli ili kufukia kashfa hiyo katika riadha.
"Nina kazi kubwa ya
kufanya kufukia kashfa hii katika nchi yangu," alisema Bolt na kuongeza:
"Kwa sasa nimeelekeza
nguvu katika hilo
na kuwadhihirishia watu kuwa mafanikio na ushindi vyote vinawezekana katika
mchezo huu."
Bolt aliyesisitiza kuwa yeye
ni mtu safi kutokana na kutowahi kupatwa na
kashfa ya kutumia dawa, lakini akasema yahitaji mtu kuwa mwangalivu sana asiangukie kwenye
mkasa huo.
Bolt, bingwa wa mbio fupi
katika mita 100 na 200, alisema kufanya kwake vizuri tangu akiwa kijana mdogo,
ni uthibitiosho kuwa yeye ni mtu safi
asiyetumia dawa za kuongeza nguvu.
"Nimewahi kuvunja rekodi
nikiwa kijana mdogo ambayo hadi sasa haijavunjwa," alisema Bolt
alipozungumza na BBC.
Nyota huyo alitumia nafasi
hiyo kuueleza ulimwengu kuwa, amekuwa akipata mafanikio kutokana na kipaji
kutoka kwa Mungu na juhudi katika mazoezi.
No comments:
Post a Comment