Kocha mpya awahofia Messi, Neymar
Gerardo Martino |
KOCHA mpya wa Barcelona , Gerardo Martino ametua rasmi Camp Nou
na
kusema utakuwa mtihani mgumu
kwake kama Lionel Messi na Neymar hawatang’ara
katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Akizungumza kwa mara ya
kwanza jana baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili, Gerardo alisema wazi ana
kazi kubwa ya kuwamudu nyota hao wawili.
Alisema kutokana na umahiri
wao, anajiona mwenye kazi ya ziada ya kuhakikisha nyota hao wawili wanacheza
kwa ufanisi katika kikosi cha kwanza.
Lakini, akajifariji kwa
kusema Neymar, aliyetua hivi karibuni kwa mkataba wa miaka mitano na Messi,
nyota bora wa Dunia mara nne, hawatamwangusha.
"Kama Messi na Neymar
watashindwa kucheza pamoja kwa ufanisi, itakuwa ni pigo kwangu kama kocha," alisema na kuongeza kuwa, jukumu kubwa
kwake kuhakikisha wanaisaidia timu kushinda.
"Naamini Barca kwa kuwa
na wachezaji hawa, itapata mafanikio makubwa. Kazi yangu ni kuwafanya wachezaji
wanifahamu na kuniamini ili kuboresha kiwango,” alisema.
Kocha huyo ambaye ni mara ya
kwanza kufundisha Ulaya, amepewa juhumu la timu hiyo kuchukua nafasi ya Tito Vilanova aliyepumzikoa kutokana na matatizo ya kiafya.
No comments:
Post a Comment