Fabregas |
Wenger: Man United hawampati Fabregas
KOCHA wa Arsenal, Arsene
Wenger amewakatisha tamaa Manchester United kuhusu kumwania Cesc Fabregas wa FC
Barcelkwa ya Hispania akisema wanajisumbua bure kwani hawatampata kwa msimu
huu.
Wenger aliyewahi kumwania nyota
huyo bila mafanikio kumrejesha Emirates msimu ujao ikiwa ni misimu miwili tangu
aondoke Emirates, alisema Fabregas hawezi kwenda Old Trafford.
Alisema hiyo inatokana na
Fabrega kutamka wazi kuwa bado anapenda kubaki Barcelona , hivyo Manchester United
wanajisumbua bure kumwania mchezaji huyo.
Alisema kwa mazingira haoni
sababu ya kuongeza dau kwa Fabregas kumzuia kwenda Old Trafford kwani anaamini
hawezi kuondoka Camp
Nou msimu huu.
Kauli hiyo inatokana na
Arsenal kukwama kumrejesha Fabregas kwa dau la pauni mil 29, hivyo hofu yake ni
kwenda Man Utd iliyo tayari kumsajili kwa pauni mil 30.
"Fabregas ameamua kubaki
Barcelona ,"
alisema Wenger mbele ya waandishi wa Habari juzi na kuongeza:
Vita ya kumwania Fabregas ni
kutokana na shauku ya nyota huyo kukosa uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza
cha Barcelona
tangu arejee akitokea Arsenal miaka miwili iliyopita.
Haya hivyo, kitendo cha
kuondoka kwa Thiago aliyetimkia Bayern Munich ya Ujerumani, kumeongeza uzito wa kubaki kutokana
na presha ya namba kupungua katika nafasi ya kiungo chini ya Kocha Tito
Vilanova.
Mapema wiki hii, Vilanova
alisema nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, angependa kubaki Camp Nou
kuboresha kiwango chake zaidi.
"Najua amepata ofa
nyingi. Lakini nimezungumza naye amenieleza angependa kubaki.
"Hana mpango wa kwenda
kwingine. Anajua kuwa hapa ndipo mahali anapoweza kucheza michuano ya kimataifa.
Ndoto yake ni kupata mafanikio hapa."
No comments:
Post a Comment