Luis Suarez |
KLABU ya Arsenal imezidi
kuonesha nia yake ya kupata saini ya mshambuliaji mtukutu Luis Suarez, raia wa Uruguay
baada ya kuongeza dau hadi pauni mil
40 ili aweze kutua Emirates.
Kiasi hicho ni nyongeza ya
pauni mil 5 ya dau la awali la pauni mil 35 ambalo lilitupwa na Liverpool licha ya nyota huyo kuonesha wazi kutaka kuhama
Anfield na kwenda Arsenal.
Habari zinasema, kwa kiasi
hicho kipya cha fedha huenda suala la mchezaji huyo likapata ufumbuzi ndani ya
saa 48 kuanzia jana kwani tayari Kocha Arsene Wenger anajiandaa kuwasilisha ofa
hiyo mpya.
Kuna habari kuwa, Arsenal
sasa imeamua kuacha mambo mengine ili kupigania usajili wa nyota aweze kucheza
Emirates msimu ujao.
Wakati Arsenal ikipambana
kusaka saini ya nyota huyo, Liverpool nayo
imekuwa ikijitahidi kumzuia asiondoke kutokana na umuhimu wake dimbani.
Mbali ya Arsenal, Suarez
amekuwa akimezewa mate na klabu kadhaa ikiwemo Real Madrid ya Hispania
Pamoja na Arsenal ‘kujikamua’
hadi kiasi cha pauni mil 40, Kocha wa Liverepool, Brendan Rodgers amekuwa akisema thamani ya
nyota huyo ni pauni mil 55 kama ya Edinson
Cavani.
Cavani ambaye pia ni nyota wa
kimataifa wa Uruguay , amejiunga
na Paris Saint-Germain tangu Jumanne wiki hii akitokea Napoli
ya Italia.
Pamoja na kauli ya kocha
huyo, hatima ya mchezaji huyo atakayekosa mechi sita za awali za Ligi Kkuu, itaamuliwa na mmiliki wa klabu hiyo,
Kampuni ya Fenway Sports
Group ya Marekani inayomiliki klabu hiyo.
Kuna uwezekano wa Arsenal
kufanikiwa mpango huo kutokana mkataba wake kuonesha kuwa hiyo ndio
thamani yake ya kuuzwa.
thamani yake ya kuuzwa.
Lakini, Liverpool
imedai kuwa suala la thamani hiyo kuandikwa kwenye mkataba, haina maana ndio
tahamni halisi ya nyota huyo kuondoka Anfield.
Hata hivyo, Arsenal inaamini
kuwa itampata mchezaji huyo ambaye amekuwa na shauku ya kucheza Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Wakati hayo yakiendelea,
Suarez anatarajiwa kujiunga na Liverpool hapo
kesho kwa safari ya kwenda
Suarez ni chaguo la kwanza la
Wenger katika msimu huu kabla ya kuangalia uwezekano wa kuwapata Gonzalo
Higuain wa Real Madrid ya Hispania na Wayne Rooney
wa Manchester United.
Kuhusu Higuain, nyota wa
kimataifa wa
No comments:
Post a Comment