Nyota huyo wa kimataifa wa
Hispania, ametua Manchester
City akiwa mchezaji wa
tatu kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao huku ikikaribia kumnasa pia mshambuliaji wa Fiorentina,
Stevan Jovetic.
Wakati ikicheua pauni mil 24
kumpata Negredo, inaweza kumpata Jovetic kwa kiasi cha pauni mil 23, hivyo hadi
sasa imetumia jumla ya pauni mil 90 kwa usajili.
Tayari Negredo (27), ameshafanyiwa
vipimo tangu Alhamisi kabla ya kujiunga rasmi na Manchester City iliyomaliza ziara yake nchini
Afrika Kusini tangu juzi ikifungwa 2-1 dhidi ya AmaZule.
Negredo ni kati ya washambuliaji
wazuri kwani katika msimu uliopita, alimaliza nafasi ya nne kwenye La Liga kwa
kufunga mabao 25, nyuma ya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Radamel Falcao.
Nyota huyo aliyeweka rekodi
ya usajili kwa klabu yake ya Sevilla, ameondoka baada ya kuitumikia kwa misimu
minne akiifungia mabao 70.
Kwa upande wa timu ya taifa
ya Hispania, amecheza mechi 14 na kuifungia mabao sita.
Akizungumzia kuhama kwake,
Negredo alisema miaka yake mine ya kucheza Sevilla ilikuwa ya furaha kubwa,
lakini wakati wa kucheza hapo, umekwisha anafurahia kujiunga na timu kubwa.
Negredo ni kama amemfuata
nyota mwingine wa zamani wa Sevilla, Jesus
Navas aliyetua Etihad mwezi uliopita pamoja na kiungo mwingine Mbrazil Fernandinho.
Negredo atakuwa akivalia jezi
namba tisa ambayo ilikuwa haina mtu tangu aondoke Emmanuel Adebayor, nyota wa kimataifa wa Togo .
No comments:
Post a Comment