NDOTO za Klabu ya Manchester United kupata saini ya kiungo Cesc Fabregas,
zimeyeyuka baada ya FC Barcelona kusisitiza kwa mara nyingine kuwa hawamtoi Camp Nou .
Licha ya Manchester United kugonga mwamba mara ya
kwanza katika kumwania nyota huyo, bado ilituma ofa kwa mara ya pili ya pauni
mil 30 na mchezaji.
Makamu Rais wa Klabu hiyo, Josep
Maria Bartomeu amewajibu Manchester United, kuwa hawapo tayari kumuuza kiungo
huyo kwa bei yoyote.
Japo Alhamisi wiki hii Kocha
wa United, David Moyes, alisema wanaendelea na juhudi za kumwania, lakini
wameelezwa kuwa waachane na bishara hiyo.
Bartomeu said: "Man United
imekuwa ikimtaka Fabregas kwa muda mrefu kwa sababu ni mchezaji mkubwa, lakini
hauzwi
Fabregas aliyecheza soka ya
utoto katika klabu ya Barcelona kabla ya
kutimkia Arsenal mwaka 2003, aliondoka Emirates Agosti 2011 na kurejea Camp Nou
kwa kitita cha pauni mil 30.
Akiwa Arsenal, mechi yake ya
kwanza ilikuwa ya Kombe la Ligi dhidi ya Rotherham
United ya Oktoba, 2003, wakati huo akiwa na umri wa miaka 16 na siku 177.
Tangu arejee Barcelona ,
Fabregas amekuwa hana raha kutokana na kukosa uhakika wa kikosi cha kwanza hadi
kutamani kuondoka, lakini kuondoka kwa Thiago kumeongeza thamani yake Camp Nou .
Ni mara ya kwanza kwa Bartomeu
kuonekana hadharani akizungumza akiwa na kocha mpya
Gerardo Martino aliyeziba
nafasi ya Tito Vilanova.
Ndoano ya kwanza ya Man
United kwa kiungo huyo ilikuwa Julai 15, walipokuwa tayari kucheua kiasi cha
pauni mil 25 ambazo zilikataliwa kabla ya kupanda hadi 30 na mchezaji.
Tangu arejee Barcelona, Fabregas
amecheza mechi 96 zikiwemo 60 za La Liga, lakini amekuwa akifunikwa na uwepo wa
nyota wengine kama Xavi (33) na Andres Iniesta (29).
No comments:
Post a Comment