Rooney aonyesha donda lake Facebook
MSHAMBULIAJI wa Man United na Timu ya Taifa England, Wayne Rooney ameweka picha zake katika mtandao wa kijamii wa Facebook zinazolionyesha jeraha katika bapa lake la uso.
Jeraha hilo alilipata katika mazoezi ya United, baada ya kugongana na mchezaji mwenzake Phil Jones na kumsababishia aikose mechi ya upinzani mkali iliyofanya United kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Liverpool.
Pia Rooney atazikosa mechi mbili za Timu ya Taifa England kwenye mechi za kufuzu kombe la Dunia zitakazoikutanisha England na Moldova ikifuatiwa na mechi Ukraine.
No comments:
Post a Comment