Hivi ndivyo klabu za Ligi Kuu England zilivyovunja rekodi ya usajili duniani
KLABU za Ligi Kuu ya England zimevunja rekodi ya matumizi katika usajili wa msimu huu kwa kutumia pauni milioni 630 kwa uhamisho wa nyota katika usajili uliofungwa rasmi Setemba 2.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kampuni ya Deloitte Sports Business Group, klabu za Ligi Kuu zimetumia jumla ya kiasi hicho ikiwa ni zaidi ya pauni mil 130 ya kiasi cha mwaka 2008, walipotumia pauni mil 500.
Kulikuwa na usajili mkubwa kabla ya kufungwa kwa usajili huo, ambapo Mesut Ozil aliihama Real Madrid na kutua Arsenal kwa dau la pauni milioni 42.4, huku United ikimtwaa Marouane Fellaini kwa pauni mil. 27.5 kutoka Everton.
"Habari ya usajili wa majira ya joto ni uwekwaji wa rekodi mpya: rekodi mpya ya matumizi makubwa ya pesa kwa klabu za Ligi Kuu ya England, ikitumia ada kuibwa na rekodi duniani," alisema Dan Jones wa Kampuni ya Deloitte.
Ada rekodi ya usajili kiangazi hiki iliwekwa kwa winga Gareth Bale, ambaye aliuzwa kwa Real Madrid akitokea Tottenham Hotspur kwa dau la pauni milioni 85.
Matumizi hayo ya klabu za Ligi Kuu ya hapa imezipiku ligi zote za Ulaya , huku klabu nyingi za ligi hiyo zikifanya mabadiliko ya makocha kwa kutoka ndani na nje ya nchi.
Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ inafuatia katika matumizi ya pesa nyingi kiangazi hiki, kama ilivyokuwa kwa Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’ ambazo kila moja imetumia kitita cha pauni mili 335.
Ligi Kuu ya Ufaransa ‘Ligue 1’ imeshika nafasi ya nne ikitumia kitita cha pauni milioni 315, huku ile ya Ujerumani ‘Bundesliga’ ikitumia kiasi cha pauni milioni 230.
No comments:
Post a Comment