Diego Godin afurahia Messi kuumia
Diego Godin |
Diego Godin mwenye jezi namba 2 akifurahia kimyakimya |
USEMI wa adui yako muombee njaa, ulidhihirika juzi pale Lionel Messi wa Barcelona alipoumizwa hadi kutoka ndani ya kipindi cha kwanza walipocheza na Atletico Madrid katika mechi ya Super Cup iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
Katika mechi hiyo ya kwanza Super Cup iliyochezwa uwanja wa Vicente Calderon, kabla ya Messi kutoka, Diego Godin alionekana kupeana maelekezo kwa mchezaji mwenzake Miranda wapi amgonge asiendelee na mchezo huo.
Katika kutimiza kilichopangwa, Messi alichezewa rafu na Miranda kiasi cha kushindwa kurejea kipindi cha pili huku nafasi yake ilizibwa na Cesc Fabregas kutokana na kupata maumivu ya mgongo na paja la kushoto.
Yaonesha wazi Godin ambaye ni beki wa Atletico Madrid, alifurahia kutorejea kipindi cha pili kwa kugonga mikono na Miranda kama ishara ya kumpongeza kwa kazi nzurialiyofanya.
Kwa upande wa Messi, si mara ya kwanza kwake kupata maumivu kama hayo kwani katika msimu uliopita, alikabiliwa na maumivu ya bega la kulia.
Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Andoni Zubizarreta, alisema maumivu ya Messi yametokana na kukanyagwa, hivyo kuongeza maumivu mguu wa kushoto aliopata maumivu madogo katika mechi ya ufunguzi wa La Liga, walipoifunga Levante 7-0.
Katika mechi hiyo, Neymar aliyetokea benchi ndie aliisawazishia Barcelona kutokana na krosi ya Dani Alves akisawazisha bao la David Villa, aliyewahi kuchezea Barcelona.
Bao la kichwa la Neymar, lilifungwa kishujaa kiasi cha kumshangaza Andoni, akisema alipiga kichwa kwenye mazingira yasiyotarajiwa.
No comments:
Post a Comment