Louis Saha astaafu soka
HAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Louis Saha jana alitumia ‘birthday’ yake ya miaka 35 kutangaza kustaafu kucheza soka.
Saha aliyewahi kuichezea Ufaransa, alianzia soka yake katika klabu ya Metz kabla ya kwenda Fulham.
Mwaka 2004, Saha alitoka Fulham na kuhamia Man Utd kwa kitita cha pauni Mil 12.8, aking’ara Ligi Kuu ya England na kutwaa tangu Ligi ya Mabingwa.
Katika msimu uliopita, Saha alikuwa katika klabu ya Lazio ya Italia akicheza mechi sita.
"Nitaachana na soka ya kulipwa, nawatakia mafanikio wachezaji chipukizi,” aliema Saha kupitia akaunti yake ya Twitter "nawashukuru makocha wote waliowahi kunifundisha, viongozi, wachezaji, wapinzani niliokutana nao wakati wote nikicheza soka, mashabiki,” alisema.
Saha aliyeichezea Ufaransa mechi 20, alikuwemo kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.
Saha ametangaza kustaafu tangu jana baada ya kufikisha miaka 35, tangu azaliwe Augusti 8, mwaka 1978
No comments:
Post a Comment