Miamba 14 kuanza Ligi Kuu Bara kesho
KIVUMBI cha Ligi Kuu Tanzania bara kinaanza kutimka kesho kwa miamba 14 kuanza kampeni ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo msimu wa 2013/14 huku bingwa mtetezi, Yanga akianza na Ashanti United ya Ilala kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Yanga chini ya kocha wake Ernie Brandts iinayoshuka dimbani ikitoka kutwaa Ngao ya Jamii
kwa kuifunga Azam FC bao 1-0 Agosti 17, itakuwa ikipigania ushindi ili kuanza vema ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom-Tanzania.
Wakati Yanga ikiwa na hesabu hizo, Ashanti United ‘Wazee wa miba,’ watakuwa wakipambana vilivyo kushinda kudhihirisha uwezo wao kisoka uliowafanya warejee Ligi Kuu pamoja na Rhino Rangers ya Tabora na Mbeya City ya Mbeya.
Yanga, bingwa mara 24 tangu mwaka 1965 ikianzia kampeni Uwanja wa Taifa, mtani wake Simba anayesaka ubingwa wa 18, atakuwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora kuwakabili wanajeshi wa Rhino Rangers wanaocheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwao mwaka 1994.
Simba chini ya Kocha Mkuu Abdallah King Kibadeni, atakuwa na kazi ya kusaka ushindi wa ugenini katika mechi hiyo inayotarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi waliokosa ligi hiyo kwa miaka 12, tangu kushuka daraja kwa timu ya Milambo FC iliyowahi kuwika na kutikisa katika enzi zake.
Wakati Simba ikisaka ushindi ili kuanza vema kampeni ya kutaka kutwaa ubingwa kusawazisha makosa ya kuangukia nafasi ya tatu msimu uliopia, Rhino Rangers chini ya Kocha wake Sebastiani Nkoma, watakuwa wakipambana kudhihirisha uwezo mbele ya mashabi na wakazi wa Tabora.
Akizungumza kuelekea mechi ya leo, Meneja ya Rhino Rangers, Marijan Idd Lukongo alisema hawakupanda daraja ili kuwa wasindikizaji bali kuleta ushindani wa kweli katika Ligi Kuu kwa
lengo la kutwaa ubingwa kama Tukuyu Stars mwaka 1986.
“Tumekuja kuwashika, hatukupanda Ligi Kuu kwa kubahatisha…kwa uwezo, tutapambana
kunatoa upinzani wa hali ya juu. Tunaomba sapoti ya mashabiki kwani tuna uhakika sio kubaki
tu, bali kufanya vizuri kama si kutwaa ubingwa kama Tukuyu Stars 1986,” alisema
Nje ya watani wa jadi, mabingwa mara mbili wa ligi hiyo, Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro itakuwa
nyumbani Manungu kuwakaribisha Azam FC, mechi inayotarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa kutokana
na uwezo wa timu zote mbili.
Azam inayotokea kufungwa bao 1-0 na Yanga katiuka mechi ya Ngao ya Janii, itakuwa na kazi ya kuonesha na kudhihirisha matunda ya kambi ya wiki mbili nchini Afrika Kusini ambako ilicheza mechi nne za kirafiki dhidi
ya Mamelodi Sandowns, Kaizer Chiefs, Moroka Swallows na
Mechi nyingine leo ni katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha kwa maafande wa JKT Oljoro kuwakaribisha Coastal Union ya Tanga huku Magambo JKT ya Tanga, ikiwa mwenyeji wa JKT Ruvu
kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Wageni katika msimu huu, Mbeya City chini ya kocha wake Juma Mwambusi, leo itakuwa kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Edward Moringe Sokoine, kuwakaribisha Kagera Sugar waliomaliza msimu uliopita wakiwa nafasi ya nne chini ya Kibadeni,
safari hii wakiwa chini ya Jackson Mayanja, raia wa Uganda.
Vita nyingine itakuwa kwenye Uwanja wa Mabatini, Kibaha, Pwani kwa maafande wa Ruvu Shoooting kuwakaribisha maafande wenzao wa Tanzania Prisons katika mechi inayotarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa timu hizo.
Raundi ya pili wa ligi hiyo utachezwa Agosti 28, kabla ya kupitisha mechi za mchujo fainali za Kombe la Dunia kati ya Gambia na Tanzania, Taifa Stars itakayochezwa Septemba 7, mjini Banjul huku raundi ya tatu ikiendelea Septemba 14.
No comments:
Post a Comment