Wadhamini Stars mwendo mdundo
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akimkabidhi zawadi ya DVD Nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja hivi karibuni |
Meneja wa bia hiyo George Kavishe alisema juzi kuwa japo
matokeo hayo si mazuri, lakini ni vizuri Watanzania wakajua kuwa mafanikio ya
soka yanahitaji subira.
“Ni vema tukumbuke
kuwa kwenye soka kuna kushinda na kushindwa,” alisema Kavishe na kuongeza:
“Tunapenda
kuwahakikishia Watanzania kuwa sisi kama wadhamini hatujakata tamaa na bado
tuna imani na timu hii na kocha Kim Poulsen, kwa hiyo tunawaomba wasife moyo.”
Alisema wakati wanalipoanza kuidhamini timu hiyo Mei, 2012
kwa kuwekeza zaidi ya sh bilioni mbili kwa mwaka, kwa muda wa miaka mitano,
walikuwa na malengo mengi likiwemo kuinua hadhi ya timu hiyo na kuhakikisha
wanaingia kambini kwa wakati muafaka.
Kavishe alisema jambo hilo ni muhimu kwa ufanisi wa timu na
mengineyo kama kulipwa vizuri na kwa wakati, kula na kulala vizuri pamoja na
usafiri wa uhakika.
“Tumejitahidi kufanya mambo haya kwani wachezaji sasa hivi
wana DVD zenye maelezo yao, tumewapa suti mpya na za kisasa na pia tumewapa
basi jipya la kisasa. Mambo haya yote pamoja na mambo wanayofundishwa na kocha
Kim yamesaidia kuleta mabadiliko makubwa,” alisema.
Alisema kuna mafanikio mazuri ya timu ya taifa ambayo
Watanzania lazima wayakumbuke kama kuzifunga timu kama Zambia, Cameroon,
Morocco na Kenya.
Kavishe alisema walipoanza udhamini, Tanzania ilikuwa katika
nafasi ya 145 kwa ubora, lakini iliwahi kufika 109 ingawa sasa inashika nafasi
ya 121.
“Haya ni mafanikio
makubwa kwani tumesogea hatua zaidi ya 40,” alisema.
Alisema safari ya mafanikio katika mpira ni ndefu na
inahitaji uvumilivu wa hali ya juu na kuongeza kuwa Kim anafanya kazi nzuri ya
kuibua vijana.
“Kocha anahitaji kuungwa mkono na sisi sote kuanzia kwa TFF,
sisi wadhamini na Watanzania wote. Tunahitaji kuangalia picha kubwa,” alisema
na kuongeza:
“Nawaomba Watanzania tuwe wazalendo wakati huu, hii ni timu
yetu na tunatakiwa kujivunia. Vyombo vya habari pia viwe mstari wa mbele
kuonyesha uzalendo.”
Alisema mechi dhidi ya Gambia itakayochezwa mwezi Septemba
ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia ni muhimu hata kama Tanzania haisongi mbele
kwani itasaidia katika ngazi za Fifa.
No comments:
Post a Comment